Huyo ni Yesu Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2023
Lyrics
Huyo ni Yesu - Ambassadors of Christ Choir
...
ni yeye huyo ni Yesu
ndiye awezaye niokoa
damu yake Yesu ndo pekee itakasayo
matumaini yangu yote ni kwake mikononi mwake ndipo napata uzima
sina uwezo mm kujitakasana
mwili huu unileteao mauti
nainua macho yangu kwenye msalaba wa Yesu
niinuliwe Calvary nichote kwenye chemchem
mchungaji mwema wokovu wetu
msaidizi tuongoze twatamani kufika msalabani ilitutuwe mizigo yetu yote.
ni yeye huyo ni Yesu
neno la Mungu aliyeumba vyote
tumaini vizazi vyote tukianzia kwao wazee wetu
jamani huyu ndiye mwamba uliotoa maji wote wenye kiu wakayanywa
alimaliza yote msalaba na alipojitoa kua sadaka kwa wadhambi
na sasa yupo mbinguni akiwa ni wakili wetu
atutetea kwa baba yake ili nasi tuokolewe
mfalme wetu njoo tunakuhitaji maishani mwetu
wewe ndie uwezaye kutuponya na majaribu ya muovu huu mwili unatusumbua lakini tumechoka Yesu njoo tusaidie
twahitaji amani itokayo kwako njoo Yesu utupe amani moyoni
sio sisi pekee etu dunia yote yakuhitaji
matukio duniani yaonyesha tulivyochoka