Tangulia Mbele Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2014
Lyrics
Tangulia Mbele - Ambwene Mwasongwe
...
lyrics
Mbele zako Ninaomba nisaidie uende mbele yangu,
Macho yangu hayaoni nini kiko mbele ...Natumaini weweee wewe umeona,
Tangulia mbele yangu bwana kanyooshe mapito.siwezi kwa ufahamu wangu nataka leo nishinde iiii
(Kama ukienda mbele yangu hakuna jambo maagumu nitashindwa, nitajiachia kama tai nikijua wewe bwana uko mbele)x2
Mbele kuna hatarii, Mbele kuna maadui, mbele kuna vitisho mbele kuna mashimoma
Mbele kuna vitaa mbele kuna ugomvi, tangulia mbele
Nikweli nimepanga mambo mengi kufanya lakini usalama wangu umebaki kwako mwenyewe
Nataka kuwa shujaa ...
Bwana nisaidie
Ila ushujaa wangu ni kukutegemea weweee
Najua hakuna shujaa pasipo na maadui n
Najua hakuna ushindi pasipo na mapambano,
Siogopi mapambano, siogopi manenoo siogopi masimango nataka kua shujaaa
Najua dhahabu safi husafishwa kwa motooo
Najua ushindi wangu utakuja nitashindaaa
(Guitar playing)
Napenda kujifunza kwa tai, niliemfananisha na weweee
Tai hujenga nyumba yakee juu ya maporomoko makali ambapo nyoka na hatari haziwezi kufika hukoo
Tai hujali makinda yakee yakiwa madogooo
(Taiii) ajengapo nyumba yake hujengea juu ya miba mikaliii, juu yake hufunika manyoya lakini anajua nini anafanyaaaa
Ukifika wakati makinda yake yamekomaaa, taii huyanyima chakula yatoke ayafundishe kurukaa
Yanapoendelea kukataa hupuliza manyoyaa
Miba alioweka huwalazimisha kutokaa...
Lengo la tai si kuyaumiza makinda yakee
Lengo la tai ni kuyafundisha kuruka juuuuuu
Yakitoka nje huyabeba mgongoni hupanda nayo juu kisha huyaachia, Yanahangaika kutafa mama yaoo, nguvu zao zikiisha mama yao hutokeza mbelee
Kwa zoezi hiloo hujifunza kurukaa ndipo hugundua nia njema ya mama yao
Nawe Bwana Mungu nibebe kama tai nguvu zangu zikiisha nibebe kama taii
Nawe Bwana wangu nibebe kama tai nguvu zangu zikiisha nibebe tai