Loading...

Download
  • Genre:Gospel
  • Year of Release:2014

Lyrics

Ndoa - Ambwene Mwasongwe

...

Mlilelewa na wazazi

Sasa mmekuwa

Ndio maana mmeamua

Kuanza Maisha yenu

Mmeacha baba na mama

Kuwa mwili mmoja

Ndoa yenu ni takatifu

Mtu asiwatenge

Bila shaka mmejifunza

Mambo mbalimbali

Japokuwa mmepitia

Vipindi tofauti

Katika yote hayo

Mshukuruni Mungu

Katika yote hayo

Mshukuruni Mungu

Kwa kuwa amewafikisha hapa mlipo

Kwa kuwa amewafikisha hapa mlipo

*

Safari yenu ya ndoa

Mmeianza kwa imani

Ndio maana mwategemea

Matokeo mazuri

Yale mtakayotatua

Mshukuruni Mungu

Na yatakayowashinda

Mlieni Pamoja

Imani yenu yote

Iwekeni kwa Mungu

Msiweke kwenye vitu

Shetani asije ona

Akipiga hivyo vitu

Imani itayumba

Imani yenu ikiyumba

Nanyi mtayumba

Na ndoa yenu nayo iyayumba

Na ndoa yenu nayo itayumba

(Tunawaombea)

Mwende mkaanze Maisha

(Mungu wenu juu)

Mungu wenu awalinde

(Mbingu zote)

Mbingu zimeshawakubali

(Neema yake)

Neema yake ikawafunike

(Yeye Bwana)

Akawe mwalimu wenu

(Mungu wenu)

Akawe mshauri wenu

**

**

Ndoa ni kama jua

Lenye mwangaza mwanana

Kila lichomozapo

Wengi hulifurahia

Watu makundi makundi

Hulisifia sana

Jua hili jua zuri

Lina faida kwa afya

Ila jua lilelile

Likifika mchana

Wengi hulalamika

Na kulikimbia

Joto likiwazidia

Wananung'unika

Joto likiwazidia

Wananung'unika

Wana sahau walilisifia asubuhi

Wana sahau walilisifia asubuhi

Jua Likifika jioni

Faraja hurejea tena

Ila bahati mbaya

Jua

Laenda

K u z a m a

Hapo sifa za Asubuhi

Huanza kusikika upya

Walovumilia mchana

Hula matunda yake

Ila Tunawaombea

Mungu awatetee

Mtakapofika mchana

Mkavumiliane

Joto likiwazidia

Mkasameheane

Msilipize kisasi

Msijekujidhuru

Mkakumbuke jioni ya Amani yaja

Mkakumbuke jioni ya Amani yaja

**

**

Kama Kuna jema lolote

Msisite kulifanya

Na Neno la msamaha

Msilicheleweshe

Mkaishi Maisha yenu

Msiige ya wengine

Epukeni mazoea

Yanaleta viburi

Tena maneno mabaya

Huharibu tabia

Kamwe msijethubutu

Kuyatunza moyoni

Ndoa ni kipindi cha mwisho

Cha Maisha ya watu

Kitumieni vizuri

Kwa kuwa ni kifupi

Maana hamjui lini kifo kitawatenga

Maana hamjui lini kifo kitawatenga

Mtendee mema mwenzako

Kadiri utakavyoweza

Moyo wako utakataa

Ila jilazimishe

Kama ukitenda wema

Huna utakachopoteza

Mtendee akiwa hai

Macho yake yanaona

Wengi. Wanajilaumu

Kuwa walikosea

Wakati wa kutenda wema

Wao waliumiza

Mungu akawatenganisha

Hawaishi pamoja

Wanatamani watende mema

Ila walichelewa

Maana wenzako hawapo tena

Maana wenzako hawapo tena

*

Mmeugusa moyo wa Mungu

Kwa kutimiza agano lake

Mungu mbinguni anasubiri

Similar Songs

+

      -   or   -

      -   or   -

      NG +234

          Please Select A Playlist

          Add New Playlist

          Share on

          Embed: Love & Light EP

          Custom Size :

          • Default
          • Desktop(300*600)
          • Mobile(300*250)

          Type :

          • HTML/HTML5 (WordPress Supported)
          Get Boomplay Premium
          for
          Payment Method
          Pay With
            Review and pay
            Order Date
            Payment Method
            Due Today
            Flutterwave
              Subscription Successful

              Congratulations! You have successfully activated Boomplay 1 Month Premium.

              Now you have access to all the features of Boomplay App.
              Payment Failed

              Please check your balance and then try again.

              You'll lose your subscription if we don't have a working payment method for your account, so please check your payment details.
              Need help? Contact Boomplay Subscription Support.
              Payment Processing...
              10 s

              Payment is being processed by . Please wait while the order is being comfirmed.

              Payment Processing
              Your order is processing, and it may take up to a few days for the service provider to handle your payment. Please kindly stay tuned and check your order status in ‘User Center’.
              About Order Status