Loading...

Download
  • Genre:Gospel
  • Year of Release:2014

Lyrics

Misuli Ya Imani - Ambwene Mwasongwe

...

Ninamkumbuka mama mmoja

Aliyekuwa na Watoto saba

Alikuwa akimcha Mungu

Akimwomba mchana na Usiku

Ulipita muda sijaonana naye

Nikaamua niende nimtembelee

Nikamkuta mama mjane amechoka

Macho yamevimba kwa kulia

Akanitazama akaniambia

Ajali imeua watoto wangu

Tazama kaburi kama matuta

Mungu hakunisazia kitu

Akanikumbusha unajua mwanangu

Wewe bado ni kijana mdogo

Usijefikiri kumwacha Mungu

Hata kama amekuumiza

Akapiga magoti akitetemeka

Akamuomba Mungu mbele yangu akisema

Kwanini uliamua kuchukua wangu tu!?

(Ee Bwana)

Mtaa mzima hukuona wengine!?

(Bwana!)

Kwa nini Ajali moja iliua wangu tu!?

(Kwanini Bwana)

Kwanini siku moja walizikwa wangu tu

(Bwana)

Kwanini huku amua hapa mtaani,

(Nauliza Bwana)

Angalau kila nyumba angekufa

mmojammoja

(Bwana)

Hata nijulize maswali mengi

(Bado wewe Bwana)

Jibu bado litabaki wewe ni Mungu tu

Najua uliniamini hili naliweza

Hivyo basi Nasema Jina lako libarikiwe Amen.

"" "" "" "" ""

Kama kawaida wanadamu

Wakanyanyua vinywa wakasema

Kila mmoja aliongea lake

Ilimradi wamvunje moyo

Wako walojifanya kuwa wana uchungu

Kumbe moyoni wa ng'ong'a

Wengine wakadiriki kusema hadharani

Alijivuna sasa kiko wapi

Mama anasema akiwa msibani

Alihisi mwili unawaka moto

Aliona kama Mungu hayupo

Dunia yote kaachwa peke yake

Waliomfariji aliwaona waongo

Hawajui uchungu wa msiba

Huzuni ilipozidi akalia sana

Asikubali kufarijiwa

Ghafla akakumbuka mtetezi wake

Kwamba Mungu wake yuko hai

Akiisha mpitisha kwenye tanuru

Mwisho atang'ara kama dhahabu

(Hee Bwana)

Ulipomchukua mume wangu Bwana

Watoto walinifariji

(Sasa Bwana)

Sasa umeamua kuwachukua wote

(Wala)

Hakunisazia kitu

(Umenibebesha)

Umenibebesha mzigo mzito sana

(Mimi Bwana)

Siuwezi peke yangu

(Bwana Bwana)

Bila msaada wako

Sitaweza mimi(Ee Bwana) naomba nisaidie

(Haleluya )

"" "" "" ""

Kama unadhanj la kwako zito

Basi sasa jifunze kwa wenzako

Maana wewe kuguswa tu na tatizo

Unanung'unika Mwaka mzima

Waweza kudhani kwamba unaumwa

Kumbe hujaona wagonjwa

Ukishawaona wagonjwa wenyewe

Unaweza kupona bila dawa

Mungu Anao watu anaowaamini

Watu Wenye misuli ya Imani

Wao Wanapopita kwenye magumu

Wanamtukuza katika hayo

Hawa ndio watu Mungu huwatumia

Kumsimangia shetani

Maana kujaribiwa kwa Imani zao

Huleta utukufu kwa Mungu

Mama anasema Mungu ni mwema

Kwa sababu amenitetea

Katika kupitia kwenye magumu

Nimeona mkono wa neema

(Haleluya)

Ashukuriwe Mungu wa watakatifu

(Mungu wa Ibrahimu)

Anayetupa kushinda

(Hata tukipita)

Hata tukipita kwenye magumu gani

(Yeye Bwana)

Hatatuacha peke yetu

(Ameahidi Yesu )

Ametuahidi atakuwa nasi

Hadi ukamilifu wa dahari ee

**HALELUYA!! **

Similar Songs

+

      -   or   -

      -   or   -

      NG +234

          Please Select A Playlist

          Add New Playlist

          Share on

          Embed: Love & Light EP

          Custom Size :

          • Default
          • Desktop(300*600)
          • Mobile(300*250)

          Type :

          • HTML/HTML5 (WordPress Supported)
          Get Boomplay Premium
          for
          Payment Method
          Pay With
            Review and pay
            Order Date
            Payment Method
            Due Today
            Flutterwave
              Subscription Successful

              Congratulations! You have successfully activated Boomplay 1 Month Premium.

              Now you have access to all the features of Boomplay App.
              Payment Failed

              Please check your balance and then try again.

              You'll lose your subscription if we don't have a working payment method for your account, so please check your payment details.
              Need help? Contact Boomplay Subscription Support.
              Payment Processing...
              10 s

              Payment is being processed by . Please wait while the order is being comfirmed.

              Payment Processing
              Your order is processing, and it may take up to a few days for the service provider to handle your payment. Please kindly stay tuned and check your order status in ‘User Center’.
              About Order Status