Loading...

Download
  • Genre:Gospel
  • Year of Release:2014

Lyrics

Kuaminiwa Na Mungu - Ambwene Mwasongwe

...

Huuuuu, yeahyeahyaa

Na kumbuka nikiwa mdogo

Mimi na ndugu zangu

Siku moja tulikaa mezani

Tulitembelewa na mgeni

Mwenye Rika kama yetu

Akaambiwa aombee chakula

Aliomba maombi mazuri

Sote tulifurahia

Sio kwamba tulikuwa hatuombi

Tulifundishwa kuomba

Japo tuliomba kwa kukariri

Wazazi wetu waliposikia

Waliyapenda maombi yale

Wakatunong'oneza wanawe

Tunataka nanyi muokoke

Muombe kama hivi

(Kwa wakati huo) Hatukujua nini maana yake

(Labda kwa kuwa) Labda kwa kuwa(kwa Kweli tulikuwa ) tulikuwa wadogo

(Ila Mungu) Kumbe Mungu(Mungu mbinguni) anafuatilia

Aliiona shauku(ya baba na Mama) ya wazazi

Leo hii tumeshaokoka

***

Nikikumbuka huwa nacheka

Wakati mwingine nalia

Njia yangu haikuwa rahisi

Nilisoma sana Neno la Mungu

Nikajitazama nilivyo

Nikajihurumia mwenyewe

Yako wapi matendo ya Mungu

Yaliyohadithiwa humu

Kwa huzuni nikaamua kufunga

Ili nimueleze

Nataka kujihuzulu huduma

Kwani majaribu kwangu hayaishi

Na ninazidi kuchakaa

Ni Bora uwape watu wengine

Mzigo huu ni mzito kwangu

Kwanza mimi ni mdogo

(Ambwene ) Je unam(Ambwene mwanangu) gomea Nani!?

(Hivi hujajua tu!?) Nimekupa(Ambwene mwanangu) kazi ya kufanya

(Hebu songa mbele) Ukishinda utavikwa taji

(Hivi hujui?) Majaribu kwako ni mtaji

(Ambwene mwanangu) Hebu songa mbele

***

Sasa nimejua siri za Mungu vile anavyotujali

Yeye huona tusivyoviona

Huviona vikwazo vilivyo mbele hapendi tuangamie

Ndio maana hutuandaa mapema

Tungefukuzaje maadui elfu

Bila kuanza na mmoja

Yeye ashikapo kipimo chake apate kutujaribu

Kigezo chake ni uaminifu

Hutumia mambo madogomadogo

Tuyaonayo halali

Ili kupima uaminifu wetu

Angetuwekaje kwenye mambo makubwa

Ikiwa madogo hatuwezi

(Nimegundua) Ni jambo moja kumwamini Mungu

(Ni kitu kingine) Yeye kukuamini

Mpaka akuite rafiki yake

Akuoneshe mbele za shetani

Akuoneshe(Kama Ayubu) mbele za shetani

Yahitaji uaminifu

Nilitiwa moyo na haya yote

Nikamwadhimisha yeye

Ni wewe Bwana

Ni wewe

Ni wewe Bwana

Ni wewe

Uliyefanya haya yote

Ni wewe

Uliyeniokoa mimi

Ni wewe

Ni wewe Bwana

Ni wewe Bwana

Haleluyaa huuuu!

Ni wewe uliyenitoa mbali

Ni wewe uliyenishika mkono

Ni wewe uliyenivusha majaribu

Ni wewe uliyeniinua

Ni wewe Bwana wangu

Ni wewe Uliyefanya yote

Ni wewe Bwana wangu

Ni wewe Jemedari wangu

Haleluya!

***

Similar Songs

+

      -   or   -

      -   or   -

      NG +234

          Please Select A Playlist

          Add New Playlist

          Share on

          Embed: Love & Light EP

          Custom Size :

          • Default
          • Desktop(300*600)
          • Mobile(300*250)

          Type :

          • HTML/HTML5 (WordPress Supported)
          Get Boomplay Premium
          for
          Payment Method
          Pay With
            Review and pay
            Order Date
            Payment Method
            Due Today
            Flutterwave
              Subscription Successful

              Congratulations! You have successfully activated Boomplay 1 Month Premium.

              Now you have access to all the features of Boomplay App.
              Payment Failed

              Please check your balance and then try again.

              You'll lose your subscription if we don't have a working payment method for your account, so please check your payment details.
              Need help? Contact Boomplay Subscription Support.
              Payment Processing...
              10 s

              Payment is being processed by . Please wait while the order is being comfirmed.

              Payment Processing
              Your order is processing, and it may take up to a few days for the service provider to handle your payment. Please kindly stay tuned and check your order status in ‘User Center’.
              About Order Status