Nifundishe Kuomba Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2021
Lyrics
Nifundishe Kuomba - Ambwene Mwasongwe
...
Jina lako Messiah
Hili ni ombi langu, Nifundishe kuomba
Nifundishe kunena, nifundishe kiasi
nifundishe imani ya matendo, nipe moyo wa toba
Nautaka uwepo unakoishi, ambako wewe ni kichwa cha kanisa.
Nazitaka nguvu ulizonazo wewe, ninataka upako
maneno yangu, matendo yamgu, tabia yangu, zifanane na hisia zako.
nikitembea nitembee na wewe Yesu, ninataka kushinda aaaiii
nami nakusalute eeeh ewe master
ninakuimbia wimbo, ninapaza sauti
nami na kusifu, kuhani wa ubora.
mmiliki halali kwa agano la neem.
jina lako ni messiah
hili ni ombi langu, nifundishe kuomba
nifundishe kunena, nifundishe kiasi
nifundishe imani ya matendo, nipe moyo wa toba
ndani ya moyo wangu, ninataka uishi wewe bwana wa wema
uewezae kuuzuia ulimi wangu, usinene sawasawa na hasira zangu.
uewezae kuituliza akili yangu, isichanganyikiwe wakati wa raha
uwezae kunituliza wakati wa shida na matatizo.
wakati wengine wakimbiapo, ukanipe jibu la mbio zao.
nguvu yako ikanizuie kwenda pale hakuna awezae niona, pale ambapo hayupo awezae sema acha, neno lako likanizuie kufanya.
neema yako ikanifanye kupakua chakula tofautu na njaa yangu.
kule nisikoweza kwenda mchana, nisaidie nisiende usiku.
yale nisiyoweza sema hadharani, nisiseme gizani.
nautaka uso wako kama wa chuma
vinyamkela wasioweza kuustahimili.
naitaka lugha ya kimbingu, isiyoneneka isiyonenwa na mtu.
natamani mbingu za mbingu kwenye neema, kule Paulo alipoogelea nguvu zako.
nikitembea, nitembee na wewe Yesu.
ninataka kushinda aaaaiiii
nitakanyaga mahali waoga hawapawezi.
nitafanya ubabe kwenye ulimwengu wa roho
nitapitisha mkong'oto kwenye mikwamo.
nitaonyesha jeuri kwa shetani
maana ufalme nauteka oooo
unatekwa na wenye nguvu aiiiii
Nami nakusalute
ninakuimbia wimbo, ninapaza sauti
nami nakusifu, kuhani wa ubora
mmiliki halali wa agano la neema
Jina lako ni Messiah
hili ni ombi langu, nifundishe kuomba
nifundishe kunena, nifundishe kiasi
nifundishe imani ya matendo, nipe moyo wa toba.