Ombi langu Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2022
This song is not currently available in your region.
Try the alternative versions below.
Alternative versions:
Lyrics
OMBI LANGU - Ambwene Mwasongwe
...
mhhhhhmhhhh haleluya!
Nakuapia Moyo, nitakulinda
Maana najua kwako, kuna chemichemi
Nitakujengea boma, uwe salama
Adui akija, asikumeze
Usiruhusu maneno, yakuvuruge
Usiruhusu hasira, zikae kwako
Nitamuweka mlinzi, awe ngome yako
Akupiganie, ubaki salama
Bwana naomba utete nao
Wale wanaoteta nami
Naomba upigane na adui zangu wote
Mimi sitaki kubishana nao,
Sitaki kupambana nao
Nisije nikakosea, wakanilaumu
Maana wameshavuta upinde
Wako kwenye mangojeo yao
Wamenuna wamekunja sura, Wana hasira nami
Kinachowafanya wasinidhuru,
Ni kwamba hawajapata sababu
Wanahesabu hatua zangu nikosee, waninase
Usiache mguu usogezwe, ninaswe kwenye mitego yao
Weka mgojezi kinywani mwangu
Anilinde nisiropoke
Heeeeee!
Hili ni ombi langu, kwako
Mungu akukumbuke, na wewe
Atembee nawewe
Hata uwapo gizani akulinde
wewe ni wimbo wangu
Tena dawa ya moyo wangu
u fahari yangu