MUNGU WA IBADA Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2021
Lyrics
MUNGU WA IBADA - Ambwene Mwasongwe
...
Wewe ni Mungu
Wewe ni Mwema
Ulikuweko Kabla ya mwanzo
Ulikuweko Kabla ya miaka
Ndiwe uliweka mbingu za mbingu
Ulimweka kerubi
Akuabudu
Akafunika kiti kwa mbawa zake
Mlima wa moto kwenye mawe ya moto
Akaabudu Utukufu ukaonekana
Ila ukatazama moyo wa kerubi
Akajichuuza akajivuna
Uovu ukaonekana ndani yake akang'olewa
Akafukuzwa ibada ikaendelea
Maana wewe ni Mungu
Mungu wa ibada
Aaaah
Ndipo ukaumba mtu kwa mfano wako na sura yako
Ndipo ukamweka bustani ya edeni
Ukamtembelea ukaongea naye
Akakuabudu uuuh Gwemaka
Wewe ni Mungu, Mungu wa ibada
~~~~°°~~~~~
***
Wewe ni Mungu
Chanzo cha vyote
Wewe ni Bwana
Injini ya vyote
Ndio maana wewe haulali
Ndio sababu wewe hausinzii
Siku ukilala itakuwa kasheshe
Maana vilivyolala vyote vitaamka
Vilivyo macho naamini vitala
Itakuwa kasheshe na mtikisiko
Dude la baharini ndipo litaamka
Nani atalifunga joka lewiathani?
Bahari itakiuka sheria iliyowekewa
Nchi itakiuka amri uliyoipa
Vitu vyote vitakwenda bila sheria
Maana mwenye sheria utakuwa umelala
Ahsante maana hulali
Ahsante maana husinzii
Wewe ni Injini ya kuendesha vitu vyote
Bwana Unaweza
Bwana una nguvu
Wewe ni Mungu (umeipa sheria bahari)
wa ibada(umeipa sheria Dunia)
Wewe ni Bwana muumba (umeipa sheria nchi)
(Bwana inakutii ardhi)
Sheria zote u wewe (umevitiisha vitu vyote vya Dunia vimelala, vimetulia)
Wewe ni Bwana wa vitu vyote
(Umempa Mwana damu mamlaka) Aaaah
(Akalala akaamka) Aaaah
(Adui alipoingia, vilivyolala vikaamka) Aaaah
Aliamsha mauti na kuzimu
Kifo kikammeza
Kikaua mwili wake
Wewe ukamuandalia wokovu
~~~~~~~~~
Wewe ni Mungu
Usiyeshindwa
Huhitaji jeshi kushinda vita
Huhitaji vingi kushibisha watu
Huhitaji mawe magumu kushinda
Daudi na mawe yake yale matano
Alitumia moja kwa Jina la Bwana
Chupa ya mafuta ilikuwa ndogo
Ila ilitosha kujaza mapipa
Watu wanne tena wakoma na visigino vyao
Wakasikizisha vishindo Kwa Jina la Bwana
Jeshi likakimbia likaachia nyara
Huhitaji mapana mengi kuwapiga watu jeuri
Kwa malaika mmoja
Wazaliwa wa kwanza walikufa
Farao alikoma akamwambia Musa Nendeni
Mkamwabudu Jehova maana yeye peke yake ni Mungu
Aaaaah
Wewe ni Mungu
Mungu wa ibada
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Bwana tubariki
Utulinde sote
Utupe Roho wako
Atuongoze kwa Yesu
Amen
Kweli atukuzwe
Yesu Ndiye Bwana tu
Yeye hutubariki
Wewe ni Mungu wa ibada
Wewe ni Bwana muumba
Sheria zote u wewe
Wewe ni Bwana wa vitu vyote
Aaaah
~~*~~
¬ ¬