NIFUNDISHE KUOMBA Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2021
Lyrics
NIFUNDISHE KUOMBA - AMBWENE MWASONGWE
...
Jina lako Messiah!
hili ni ombi langu
nifundishe kuomba
Nifundishe kunena
Nifundishe kiasi
Nifundishe imani
Ya matendo
Nipe moyo wa toba
Nautaka uwepo wako
Unakoishi
Ambako wewe ni kichwa cha kanisa
Nazitaka nguvu ulizonazo wewe
Ninataka upako
Maneno yangu
Matendo yangu
Tabia yangu
Zifanane na hisia zako
Nikitembea nitembee
Na wewe Yesu
Nina taka kushinda
Nami nakusaluti(wewe master)
Ninakuimbia wimbo
Ninapaza sauti
Nami nakusifu (Kuhani wa ubora)
Mmiliki halali
Wa agano la neema
Jina lako messiah
Hili ni ombi langu
(Hili ni ombi langu) nifundishe kuomba
Nifundishe kunena
Nifundishe kiasi
Nifundishe Imani ya Matendo
Nipe moyo wa toba
Ndani ya moyo wangu
Nina taka uishi wewe Bwana wa wema
Uwezaye kuuzuia ulimi wangu
Usinene Sawa Sawa na hasira zangu
Uwezaye kuituliza akili yangu isichanganyikiwe wakati wa raha
Uwezaye kunituliza wakati wa shida na matatizo
Wakati wengine wakimbiapo
Ukanipe jibu la mbio zao
Nguvu yako ikanizuie kwenda
Pale hakuna awezaye niona
Pale ambapo hayupo awezaye sema acha
Neno lako likanizuie kufanya
Neema yako ikanifanye kupakua
Chakula tofauti na njaa yangu
Kule nisikoweza kwenda mchana
Nisaidie nisiende Usiku
Yale nisiyoweza sema hadharani
Nisiseme gizani
Nautaka uso wako
Kama wa chuma
Vinyamkera wasiouweza kustahimili
Naitaka lugha ya kimbingu isiyoneneka
Isiyonenwa na mtu
Natamani mbingu za mbingu
Kwenye neema
Kule Paulo alikoogelea nguvu zako
Nikitembea nitembee na wewe Yesu
Nina taka kushinda
(Heei) nitakanyaga mahali waoga
Hawapawezi
Nita fanya ubabe
Kwenye ulimwengu wa roho
Nitapitisha mkong'oto kwenye mikwamo
Nitaonyesha jeuri kwa shetani
Maana ufalme nauteka ooh
Unatekwa na wenye nguvu
Nami nakusaluti (ewe master)
Nakuimbia wimbo
Ninapaza sauti
Nami nakusifu
Kuhani wa ubora
Mmiliki halali
Wa agano la neema
Jina lako messiah
Hilo ni ombi langu
Nifundishe kuomba
Nifundishe kunena
Nifundishe kiasi
Nifundishe Imani ya matendo
Nipe moyo wa toba