Mamlaka Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2023
Lyrics
Mamlaka - Nay Wa Mitego
...
Kuna wengine wanaumwa asante niko fresh
Wengine wamekufa kuna sababu mi kuishi
Umenipa nyota yakupendwa na watu sio laisi
Umefanya mitaa iseme nafaa kua rais
Umenipa sauti ya mamlaka ( wewe)
Umenitoa hofu na mashaka (ni wewe)
Kila ninaposimama wanafyata (wewe)
Mi naomba siku moja siku yako ya mamlaka
Naomba siku yako moja niwe rais wa nchi nzima
Wananchi nawapa umeme ila kwa viongozi nazima
Siku yako moja ya mamlaka walimu sitowatupa
Nawapa mishahara wabunge mambo yao yawe supa
Alafu sasa kazi ya ubunge itakua ni wito
Wabunge watachukua mishahara ya walimu yani simple
Bungeni wataenda kwa bus walimu wanaendesha V8
Nasitotaka mjadala mana haitokua dibeit
Kuna mbunge bila mwaimu (aah wapi)
Kuna daktari bila mwakmu (aah wapi)
Kuna waziri bila mwalimu (aah wapi)
Nauliza hivi kuna rais bila mwalimu (aah wapi)
Siku yako moja tu hakimu atakua mfungwa
Ili ajue uchungu wakusingiziwa na ukafungwa
Washikaji zangu police nitawaongezea vibunda
Ili msile rushwa kisa mshahara wa kuunga unga
Iwe iwe iwe iwee
Iwe iwe iwe iwee
Iwe iwe iwe iwee
Siku ya mamlaka
Iwe iwe iwe iwee
Iwe iwe iwe iwee
Iwe iwe iwe iwee
Siku ya mamlaka
Kwenye hiyo siku kuna jambo ukilifanya utanibeba
Wanawake watafute kwa jasho na wanaume waende leba
Please husinipe uwezo wakumgeuza mwanadamu mbuzi
Mana mbuzi watakua ni wengi binadam ana maudhi
Siku yako moja ya mamlaka
Tajiri awe masikini masikini awe tajiri
Alieshiba atamkumbuka mwenye njaa we niamini
Ninachotaka waheshimiane kati ya wajuu na chini
Naomba siku yako moja viongozi waishi maisha ya wapiga kura
Na wapiga kura waishi maisha ya viongozi
Nataka waone masikini wanatesekaje
Na ahadi zao za uongo wanazotoa zinaumaje
Sikiza baba husinichoke mwanao
Siku moja ya mamlaka japo nnamambo kibao
Ccm wawe chadema chadema wawe ccm
Wapo watajifunza kitu na kua na ubinadamu
Alafu naywamitego awe basata basata wawe wamitego
Na wakitoboa nafa
Naomba baba mkuu nipe siku moja tu
Niwapokonye wenye magari niwape watembea kwa mguu
Kuna maisha bila siasa (aah wapi)
Tuseme maisha sio siasa (aah wapi
Vipi simba bila yanga (aah wapi)
Mgonjwa bila mganga (aaah wapi)
.......
Iwe iwe iwe iwee
Iwe iwe iwe iwee
Iwe iwe iwe iwee
Siku ya mamlaka
Iwe iwe iwe iwee
Iwe iwe iwe iwee
Iwe iwe iwe iwee
Siku ya mamlaka