Wambea Lyrics
- Genre:Singeli
- Year of Release:2023
Lyrics
Wambea - Balaa Mc
...
(Vinanda classic)
Wololilo liloliloliloliloo... aah Chunchu eeh
Kataa, kataa hujasema
Eti huyu na yule mtu na demu wake
Eti mkikaaga mnabusiana
Na mnakwilikwichi, ah sjasema mimi, wala sio mimi
Heh! mimi tena? Mnanisingizia
Ni huyu na bwana wake, wanakusemaga
Eti mnavyopendana mnajishaua
Waone kwanza umbea tu, ndo unawasumbua
Hamna lolote, na yenu kuniharibia
Mwone kwanza bichwa kubwa, ndo unachokijua
Kushinda vibarazani kuongelea usiyoyajua eti so mimi, nyo!
Unanibania pua, Mwone kwanza umbea tu
Ndo unakusumbua
Waone kwanza wambeaaa
Kaeni vizuri, tena mtulie (Wambeaaa)
Mjipange vizuri msinikurupukie (Wambeaaa)
Kaeni vizuri, tena mtulie (Wambeaaa)
Wambea wangu kwanza hongereni
Na mnaonifatilia poleni kwa safari
Nahitaji kuwaambia yamenijaa mdomoni
Kwa huyu nilie naye kumwacha sizani
Mtafanya juu na chini kazi bure
Kunitoa mimi mh, labda mniuee
Vinginevyo nyi ndo mtakuwa misukule
Mna viherehere ka vinyago vya mpapure
Sasa skieni, nataka penzi letu litrend
Mtufatilie hakikisheni tuwe Zuchu na Daimondi
Nyie si wambea eh, mi nawalipeni
Na mkifanya kazi vizuri nawasajili kwa kampuni
Halafu nimesahau inabidi mpate vifaa
Mana mpo serious, kila nikiwakataa
Inabidi mpate sim kamera mpige na picha
Oya Bodi wape maji wanywe, washapumzika
Mambo bado, tuendelee na vita
Waone kwanza wambeaa
Kaeni vizuri, tena mtulie (Wambeaaa)
Mjipange vizuri msinikurupukie (Wambeaaa)
Kaeni vizuri, tena mtulie (Wambeaaa)
Zidisheni ila tu msituharibie (Wambeaa)
Kaeni vizuri, tena mtulie (Wambeaaa)
Mjipange vizuri msinikurupukie (Wambeaaa)
Kaeni vizuri, tena mtulie (Wambeaaa)
Zidisheni ila tu msituharibie
Huyu ni wangu, nimemchagua kama nimempenda mi basi hakuna wa kupindua
Mkiingia kumi na nane zangu ndo mtanijua mana ntakachofanya Mungu ndo anaejua
Nasemaje, Staki masihara na mke wangu, tutagombana
Kunifatilia familia Nasemaje, tutauwana
Aloo we! Tutazagamuana
Najua inauliza kwa njia gani ila tutajuana
Kataa, kataa hujasema
Eti huyu na yule mtu na demu wake
Eti mkikaaga mnabusiana
Na mnakwilikwichi, ah sjasema mimi, wala sio mimi
Heh! mimi tena? Mnanisingizia
Ni huyu na bwana wake, wanakusemaga
Eti mnavyopendana mnajishaua
Wao inawauma, ah inachoma!
Mnapendana sana
Acha bahariaaaaaa
Aah Balaa MC 26kipaji eh
Aah nikiwa vinanda classic
Aah nikiwa Producer Fadhili Chunchu chungchang
Ah timu ile ile 26Kipaji eh
Nakubali sana Meneja ***
****************
****************
****************