Milma Ya Kwetu Lyrics
- Genre:Alté
- Year of Release:2019
This song is not currently available in your region.
Lyrics
Milma Ya Kwetu - Ruby Tz
...
Nikiitazama Milima ya kwetu
machozi yanitoka kwa uchungu na mawazo
Tulitoka wawili ninarudi peke yangu
baba na mama wataniuliza mume wako yuko wapi
Ndugu na jamaa wataniuliza mume wako yuko wapi eeh
Nitasema nini kwa baba mimi najuta ooh
kwa pesa zake nyingi alizopoteza yeye
Harusi ilifanyika kwa gharama kubwa sana
Watu walikula na kunywa na kusaza maama
nikaenda kuishi na bwana yule mjini
kazinyake ilikua ni vituko
kazi yake ilikua ni vitimbwi
Akaanza kuchelewa akienda kazini
nikimuuliza anitukana hadharani
aibu..
Kuna bibi alikuja hadi mlangoni
kujitetea akisema shemeji yake kaja
aaah
Hatimaye kunibeza na kunidharau
Shikamoo ikaisha ikabaki
vipi wewe mambo zako, vipi wewe mambo zako weewe
Walisema dalili ya mvua ni mawingu
Niliyempenda kanitoroka aah
kanitoroka nateseka
Walisema dalili ya mvua ni mawingu
Niliyempenda kanitoroka aah
Nilinyang'anywa tonge kinywani mimi ooh
Nilinyang'anywa tonge mdomoni mimi ee
Niliyempenda kanitoroka mama yo yoo
niliyempenda kanikimbia masikini masikini
nifanye nini
Walisema dalili ya mvua ni mawingu
Niliyempenda kanitoroka aah
kanitoroka nateseka
vituko.. vituko vya bwana yule ooh
sitaweza kusahau mimi mama ooh
sitaweza kusahau mimi Ruby ee
Alikua kama helicopter ndege isiyochagua pa kutua we
kila mtaa hapa mjini jamani tazameni hana binti mmoja wala wawili mama mama
nifanye
Walisema dalili ya mvua ni mawingu
Niliyempenda kanitoroka aah
kanitoroka nateseka
Walisema dalili ya mvua ni mawingu
Niliyempenda kanitoroka aah