Hey Lord ft. Mzungu Kichaa Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2009
Lyrics
Hey Lord ft. Mzungu Kichaa - Fid Q
...
nyumbani ndg wanauwana
ili warithi mali
jela wanafungana wakati undg kufaana
najiuliza swali kisha napata jibu
nakubali kuwa maisha hayawi bila ubandidu
palipo maslahi usisite kuamua kuaribu
ingali yuhai utatubu dhambi taratibu
mwanadam amemtawala mwenzie kwa kumuumiza
na kuua mpaka asivyovihitaji bila kubakiza
hii inafanya nafsi yangu ikose subira
ilikosa usingizi woga huzuni na hasira
hakuna kampeni za ukimwi nia ni kuuza mipira tu
chanzo cha vita nyingi sasa ni kupeana ajira tu
misaada haitoki bila kudhalilishwa
ngos zinalipa maskini kisha wanapiga picha
uchumi uliopo haupo kwa maslahi ya wengi
siasa imegeuka uhuni baadhi ya viongozi ni wezi
ukistuka kuona chupi utazimia ukiona mlima
siku kuu nipe bunduki staki zabibu au Dina
staki nguo ya siku kuu nipe gwanda niende chimbo kiana
mitaa inanipa ujuzi uwezo pia ilinipa jina
haihitaji ufanye uchunguzi ili upate maelezo ya kina
mi ni wa mwisho kulala pia ni wa kwanza kuamka
usiku kucha huaga najibanza kwenye ukuta
sina shuka labda kama nmevuta kigoli
sina mzuka nastuka hata cha ukucha nambonji
au nanusa chupa ya gundi au petroli
nakesha kama bundi sanjari na walinzi wa lorge
maisha yangu yako ovyo na nnavumilia msoto
naona poa kuliko yale ya kwenye vituo vya watoto
vyakula vibovu havifai kwa matumizi wasimamizi wanabaka mabinti sababu ya chips
sikuwa na jinsi zaidi ya kuamua kurudi street
tunageuzwa mahouseboy na wanaozuga kutuadopt
ukijifanya uko too big wanaku2pac
mi ni zaidi ya mtafutaji ndo mmana sipumziki
polisi wamepanda chati sababu tu ya