Loading...

Download
  • Genre:Bongo Flava
  • Year of Release:2003

Lyrics

Kikao Cha Dharura - Professor Jay

...

Professor Jay ft. Babu Ayoub

Kikao cha Dharura     


VERSE 1


Prof Jay:

Nawashukuru sana wananchi kwa kweza kunipa kura 

Nashangaa nimeitwa ghafla kwenye kikao cha dharula 

Kikao kinaashiria kina maswali juu yangu 

Hii inatokana na ndiyo mzee na ahadi zangu..


Naona watu ni wengi wananchi walio na maana 

Najaribu kutafakari ni nini kinawachanganya!!


Nipo tayari kujibu maswali yenu zamu kwa zamu 

Watakao uliza maswali na ningependa niwafahamu


Swali:


..Naitwa sajent Byemero kwa niaba ya jeshi la polisi 

Nilikuwa nauliza zile helikopta zetu vipi?


Jibu:


Prof Jay:

Nafikiria kwanza kuanzisha chuo cha marubani 

Vinginevyo mtapata ajali nyingi sana angani. 

Baskeli hamjui kuendesha helikopta mtaendeshaje

Kila mtu aendeshe yake huko angani itakuwaje?


Swali:


Mheshimiwa sisi wakulima ulituahidi matrekta 

Na siku zinayoyoma tu mbona haujayaleta ?


Jibu:


Prof Jay:

Wakulima mngeendelea tu kutumia jembe la mkono 

Serikali haina hela bajeti imefika kikomo 

Naona kilimo cha mkono kiniendelea vizuri 

Jamani kazeni mikono endeleeni kukaza misuli


KIITIKIO


Wananchi tupo pamoja hapo. (siyo mzeeeeeee)

Watanzania tunaerewana kule, (siyo mzeeeeeee)

Washika dau na wapiga kura pale (siyo mzeeeeeee)


Eeehh: siyo mzee....eti, (siyo mzeeeeeee) 

Wakulima tupo pamoja pale, (siyo mzeeeeeee) 

Wanafunzi tunaelewana kule, (siyo mzeeeeeee) 

Mabahamedi na mapolisi pale (siyo mzeeeeeee)


VERSE 2


Prof Jay:

Mabaaamedi ondoeni hofu kilio chenu nimekisikia 

Ma benzi yenu yapo bandarini tayari yameshawadia 

Nimemchagua kiranja ili anipe idadi yenu 

Niwape funguo zenu muondoke na magari yenu.


Swali:


Ulituahidi utatujengea barabara tano tano juu na chini

Hizo zote hatutaki tunataka moja tu ardhini

Kila siku tunapita barabara zinakuwa mbaya 

Umeyafumbia macho mheshimiwa huoni haya?


Jibu:


Prof Jay:

Barabara ya makwekwe nimesha imwaga kifusi 

Baada ya wiki mbili itakuwa safi kama urusi

Makandarasi wanafanya kazi kutoka china na madagascar 

Kuhusu vibarabara naomba muondoe shaka.


Swali:


Eeh vipi mzee mabomba kutoa maji na maziwa nchi nzima ?


Jibu:


Prof Jay:

Jamani naomba muulize maswali ya utu uzima 

Mabomba kutoa maji na maziwa haiwezekani 

Mlinukuu vibaya nasisitiza haiwezekani


Swali:


Mzee hali ni mbaya si tungegawana vya kwako? 

Kwenye kampeni zako si ilikuwa moja ya ahadi zako ?


Jibu:


Prof Jay:

Eeehh? kugawana vya kwangu hilo swala litakuwa gumu 

Familia itanitazama ebo? nina majukumu 

Imeandikwa kila mtu atabeba msalaba wake 

Kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake 

Mbona mnaniuliza maswali mengi kunikomoa 

Jamani watanzania tunajenga tunabomoa


RUDIA KIITIKIO x2


VERSE :3


Prof Jay:

Wafanyakazi wa serikalini sasa nyinyi magari ya nini?

Daladala chungu mzima mnaweza kuwahi kazini 

Nasema mnapenda sana starehe kuliko kazi 

Na hiyo ndio sababu mnaharibu hiki kizazi.


Wanafunzi niliwahidi mtafanyia practical mwezini 

Kabla ya kupeleka mi nilifanya utafiti 

Nimengundua huko mwezini kweli kuna baridi sana 

Na pia kunavitisho kuwepo kambi za osama


Mkinichngua tena mtakwenda huko mapema 

Nanita tekeleza kila neno ninalo sema


Sema nimesongwa na haka kamuda 

Mkiniongezea muda kila kitu babu kubwa 

Wengine kimya na maswali yamepungua 

Yeyote mwenye swali ningependa kumtambua.


Naona mnanong'ona na wengi mmekunja sura 

Hii inaonyesha mmeridhika kunipa kura 

Nadhani ndugu zangu tuko pamoja...... (aagh wapi) 

Jamani tupunguzeni jazba basi kidogo...... (hatutaki)


Sasa watanzania mbona mnaazisha vurugu 

Nadhani mmesahau watanzania wote ni ndugu


Babu Ayoub:

Eeeh? jamani nasema hivi kikao kimeahirishwa 

Jamani maafande..... Afande miraj.... Afande mzafalu,

afande nani Gondwe njooni mtusaidie huku.

More Lyrics from Professor Jay Songs

Similar Songs

+

      -   or   -

      -   or   -

      NG +234

          Please Select A Playlist

          Add New Playlist

          Share on

          Embed: Love & Light EP

          Custom Size :

          • Default
          • Desktop(300*600)
          • Mobile(300*250)

          Type :

          • HTML/HTML5 (WordPress Supported)
          Get Boomplay Premium
          for
          Payment Method
          Pay With
            Review and pay
            Order Date
            Payment Method
            Due Today
            Flutterwave
              Subscription Successful

              Congratulations! You have successfully activated Boomplay 1 Month Premium.

              Now you have access to all the features of Boomplay App.
              Payment Failed

              Please check your balance and then try again.

              You'll lose your subscription if we don't have a working payment method for your account, so please check your payment details.
              Need help? Contact Boomplay Subscription Support.
              Payment Processing...
              10 s

              Payment is being processed by . Please wait while the order is being comfirmed.

              Payment Processing
              Your order is processing, and it may take up to a few days for the service provider to handle your payment. Please kindly stay tuned and check your order status in ‘User Center’.
              About Order Status