Loading...

Download
  • Genre:Bongo Flava
  • Year of Release:2001

Lyrics

Ndio Mzee - Professor Jay

...

Ndiyo mzee

Nimekubali

Naam ndugu wananchi, MC wenu Babu Ayubu,

Ninawaleteeni *habali japo kwa kifupi kuhusiana na huyu mgombea wetu bwana Joseph Haule

Mpeni *kula za ndiyo kwasababu yeye ni mpenda watu, ni mpenda amani,

Na ni mtu mwenye huruma kwa wananchi wote,

Kwa hivyo basi nawaomba ndugu wananchi, mumpe kula ili aingie.

Naam basi, hivyo basi ndugu wananchi,

Eeh tafadhali *namkalibisha mgombea wetu,

Bwana Joseph Haule, ili aje aweza kuzungumza na wananchi,

Karibu.



Oke Oke,

Naitwa Joseph Haule,

Mwana wa Msulopo Kianzi,

Nadhani nimeletwa niokoe hiki kizazi,

Mimi ni mwanasiasa niliyebarikiwa na Mungu,

Nimeletwa kwenu na Bwana niwapunguzie machungu,

Mimi ni mteule kusini mwa jangwa la sahara,

Ndiyo maana nimetunukiwa cheti cha juu cha utawala,

Na hekima kuliko Mfalme Suleiman--msiwe na wasi

Na hili nitalidhihirisha pindi mtakaponipa nafasi,

Actually, mimezamiria kuwasaidia,

Taifa lenye nguvu duniani liwe Tanzania,

Jamani, makofi tafadhali basi jamani!



[makofi, shangwe, nderemo na vifijo]



Ni mambo madogo tu,

Nadhani nitarekebisha mkinipa visiku vichache tu,

Uchumi utapanda ile ghafla bin-vuu,

Nataka mpaka Matonya afundishe chuo kikuu,

Nchi ya Tanzania itang’ara ile kishenzi,

Na nitahakikisha kila baamedi anamiliki benzi,

Si mtafurahi dada zangu jamani?

Ndiyoooooo

Basi endeleeni kunisifu kwa nyimbo na mapambio,

Nipeni hiyo nafasi jamani, hamwoni hali ni mbaya?

Nataka kuigeuza Tanzania kama Ulaya,

Cha kwanza nitakachofanya nitafuta umaskini,

Wanafunzi mkafanyie practical mwezini,

Kwenye mahospitali nitamwaga dawa kama mchanga,

Na nitafungua akaunti kwa kila mtoto mchanga,

Mabomba yatatoa maji na maziwa nchi nzima,

Watu wa vijijini mtasahau habari za visima,

Nitafadhili wachawi waweze kutengeneza ndege,

Kila mtu awe na yake Makonda na wapiga debe.


Si mtafurahi watanzania jamani?

Ndiyo mzee

Si ni kweli nakubalika jamani?

Ndiyo mzee

Basi mimi mkombozi wenu jama,

Ndiyo mzee

Na nitafuta shida zenu zote,

Ndiyo mzee

Hivi ni naninii, ni vijimambo,

Ndiyo mzee

Na vinanikera kwelikweli mimi,

Ndiyo mzee

Basi hali itabadilika, sawa?

Ndiyo mzee

Na hatamu tutaishika oke?

Ndiyo mzee


Wafanyakazi wa serikalini nashangaa hamna magari,

Yaani hata mikweche, hehe! Hii ni hatari,

Ninampango wa kuongeza mishahara iliyominono,

Mara mia ya ile ya mwanzo iliyofanya mfanye migomo,

Nitawapa nyumba nzuri na magari ya kifahari,

Watu watashangaa mtakapopita kila mahali,

Mkulima kila mmoja nitampatia trekta,

Nadhani hiyo kidogo itasaidia kunyanyua sekta,

Mtauza nafaka zenu bilioni kwa mabilioni,

Watu midomo wazi kama wamekamatwa ugoni,

Walimu zawadi zenu oh nimezificha moyoni,

Nadhani mtazimia siku mkizitia machoni,

We acha tu, mtafurahi nyinyi,

Ila hapo hapamfai mtu mwingine niwekeni mimi,

By the way, polisi wote mi nawasifu,

Jinsi mnavyokwenda sahani moja na wahalifu,

Sasa kila mmoja nitampatia helikopta,

Nadhani hiyo wote hapo hamjawahi kuota,

Raia wa Tanzania mtalala milango wazi,

In fact, nina uhakika wa kudhibiti ujambazi,

Nitajenga barabara tano-tano juu na chini,

Nitajenga kumbi nyingi sana za starehe baharini,

Ninaupendo kuliko mshumaa, kumulikia wenzangu,

Mtakaoyumba kiuchumi, tutagawana vya kwangu.


Si mtafurahi wa Tanzania jamani?

Ndiyo mzee

Si ni kweli nakubalika jamani?

Ndiyo mzee

Basi mimi mkombozi wenu jama,

Ndiyo mzee

Na nitafuta shida zenu zote,

Ndiyo mzee

Hivi ni naninii, ni vijimambo,

Ndiyo mzee

Na vinanikera kwelikweli mimi,

Ndiyo mzee

Basi hali itabadilika, sawa?

Ndiyo mzee

Na hatamu tutaishika oke?

Ndiyo mzee


Ndugu wananchi, kuna mtu ana swali kutoka kwa mgombea?

Nauliza hivi, kuna mtu ana swali? Basi ajitokeze ili aweze kuuliza swali



Nyie ndugu zangu huyu msimpe uongozi--siyo vizuri,

Muongo tu, mfakini na kiburi kimsuli,

Anaongopea saana! Sijui kazaliwa muda gani, alfajiri au alasiri?

Wakati mvua zile, za kipendi kile?

Amepita pita skuli lakini mambo yake si mazuri,

Wala tusimtetee, atatuangamiza,

Labda tusubiri kwanza uchaguzi umwekwisha,

Tumemfuma wenyewe kwa kalumanzila anasafishwa,

Kalumanzila akamwambia, ehe, shida yako?

Elezea fasta fasta kabla jini hajapanda,

[chafya]

Hajakaa vizuri mashetani si yakamuanza!

‘kamsukuma kwa kasi ya kimbunga amejichanja,

Tulimsikia akisema kwa sauti kubwa ya kukarikia,

Waungwana! Munisaidie! Ndiyo, sitamwelewesha!

Uongo mtupu babake ameibiwa,

waungwana wamempeleka chau mpaka kaibiwa,

Yupo-hamna gepu na pugu! Amewehuka! Hajatulia huyu mpepeeni!

[uphh uphh]

Ni sauti iliyosikika kutoka kwa mzee wa pembeni,

Sijui msaidizi mganga au mpelelezi,

Na kwa taarifa yako uongozi hupati ng’o!

Labda urudi kwenu uende ukavunje tunguri,

Na hao waganga wako waeleze hupati kitu apa,

Hata utoe chapaa


[makofi, shangwe, nderemo na vifijo]



Je wananchi mmenisikia?

Ndiyo mzee

Kwa huyu jamaa hatufai,

Ndiyo mzee

Haina vibaya uchukia,

Ndiyo mzee

Hatumtaki aondoke zake,

Ndiyo mzee

Tusimkubali na maneno yake,

Ndiyo mzee

Tunahakikisha ‘atumchagui,

Ndiyo mzee

Kwasab’ jamaa ni mnafiki,

Ndiyo mzee

Asitufanye tuwe na dhiki,

Ndiyo mzee


[makofi, shangwe, nderemo na vifijo]

More Lyrics from Professor Jay Songs

Similar Songs

+

      -   or   -

      -   or   -

      NG +234

          Please Select A Playlist

          Add New Playlist

          Share on

          Embed: Love & Light EP

          Custom Size :

          • Default
          • Desktop(300*600)
          • Mobile(300*250)

          Type :

          • HTML/HTML5 (WordPress Supported)
          Get Boomplay Premium
          for
          Payment Method
          Pay With
            Review and pay
            Order Date
            Payment Method
            Due Today
            Flutterwave
              Subscription Successful

              Congratulations! You have successfully activated Boomplay 1 Month Premium.

              Now you have access to all the features of Boomplay App.
              Payment Failed

              Please check your balance and then try again.

              You'll lose your subscription if we don't have a working payment method for your account, so please check your payment details.
              Need help? Contact Boomplay Subscription Support.
              Payment Processing...
              10 s

              Payment is being processed by . Please wait while the order is being comfirmed.

              Payment Processing
              Your order is processing, and it may take up to a few days for the service provider to handle your payment. Please kindly stay tuned and check your order status in ‘User Center’.
              About Order Status