Loading...

Download
  • Genre:Bongo Flava
  • Year of Release:2003

Lyrics

Msinitenge ft. Q-Chief - Professor Jay

...

kweli me Nina akili yakwamba nimeadhirika..

Mbio ziko ukingoni duniani nataabika..

Afya yangu inayumba nahara nakutapika..

Napiga goti natubu najuwa saa itafika..

Baada tuu yakupima nikagundua sio mzima..

Nasasa ninajukumu lakuokoa jamii nzima..

Hakuna asiyetambua gonjwa hili nilahatari..

Nilichofanya ndugu zenu niliwapasha habari..

Wengi walinitazama kwa macho yachinichini..

Ety kwakuwa ninaupungufu wakinga mwilini..

Nakila muathirika wanasema amefanya ngono..

Nahii ndio sababu iliyonifanya nifungue mdomo..

Wengi wanasahau bado wanachangia sindano..

Viwembe namikasi hospitali viwe mfano..

Watoto wameupata kupitia baba na mama..

Wazazi wanapokufa jamii inawasakama..

Na hii inatokea shuleni ama nyumbani..

Poleni wote mnaotengwa na watu njiani..

Ipo siku itafika milango itafunguka..

Na maumivu makali yadunia tutayaepuka..

CHORUS:

Msinitengee ndugu zangu msinitengee..

Msinitengeee rafiki zangu msinitengee..

Siku ikifikaa ikibidi nipumzikee..

Kwenye makazi mapya nipelekeni nipumzike nimechokaa..×2 (jamaa)


Nakwenda hospitali watu wanantazama..

Nashindwa kutembea manesi wanantukana..

Nguvu zinaniishia mwili wangu wote unanuka..

Nani wakunishika japo anifunike shuka..

Mwili wote unawasha sioni pakujikuna..

Nawaomba msaada watu wote naona wananuna..

Nikune hata kwa mti japo unipunguzie uchungu..

Namimi nitakuombea upate tawabu kwa Mungu..

Macho yamefunguka lakini mbele sioni..

Taswira yajinamizi inatokea ndani ya mboni..

Watu wenye imani wananisalia kwenye kitanda..

Wenye roho nyepesi wameshaninunulia sanda..

Wafitini nawenye chuki kwa wingi waja kuniona..

Nadhani wanafarijika kwa hali wanayoiona..

Nawatazama usoni wengine wananicheka..

Kipi mnachocheka wakati me nateseka..

Bora msingekuja mfanye party mburudike..

Waacheni wazazi wangu machozi yawabubujike..

Nakama mmenichoka ni kheri mnimalizie..

Ili maumivu makali kesho yasijirudie..

Ilanawakumbusha yakwamba safari ni moja..

Nawacha niwatangulie niendapo nitawangoja..

Hakika furaha yenu yasasa itakuwa kilio..

Nakila mmoja wenu atazikwa kwa mapambio..

CHORUS:


Msinitengee ndugu zangu msinitengeee..

Msinitengeee rafiki zangu msinitengeee ..

Siku ikifikaa ikibidi nipumzike..

Kwenye makazi mapya nipelekeni nipumzike nimechokaa×2 (jamaa)


Walimwengu nawauliza mbona mnaangalia pembeni..

Jamani mpo huru kama mnadukuduku semeni..

Nashangaa wengi wenu mnafurahi kuniona hivi..

Na ety kila mmoja anajiuliza mbona sifi..

Najuta ila kamwe nasema sijutii kufa..

Najutia nafsi yangu adhabu itakayoikuta..

Wengi mnadharau sana wagonjwa wa ukimwi..

Mnanicheka mimi mbona nanyinyi hampimi..

Aah..kama unajali nibora upitie angaza..

Okoa kizazi chako chaboko kwakujitangaza..

Ninani aliyekwambia condom inazuia ukimwi..

Naona wanajaribu kukausha bali kwa ulimi..

Ukimwi hauzuiliki hata kwa condom za bati..

Na dawa ni moja tu,,nasema acha uasherati..

Wengi naona wanakuja tu,,wapate chakuongea..

Wengine mali zangu wameshaanza kuzigombea..

Aah..nikipata nafuu wengi mnachukia..

Bado najiuliza wangapi mtanifukia..

Ninani aliyewatuma hapa hospitali mnifate..

Maana nikiwashika mikono mnatema mate..

Huwezi kuambukizwa kwakumshika muathirika..

Napale wanaponitenga najiona ndani yagharika..

Ndio maana wasionaakili wanataka kuusambaza..

Wanatoa hela nyingi ninani wakuwakataza..

............#Hamxo Tozzey tozzy

Similar Songs

+

      -   or   -

      -   or   -

      NG +234

          Please Select A Playlist

          Add New Playlist

          Share on

          Embed: Love & Light EP

          Custom Size :

          • Default
          • Desktop(300*600)
          • Mobile(300*250)

          Type :

          • HTML/HTML5 (WordPress Supported)
          Get Boomplay Premium
          for
          Payment Method
          Pay With
            Review and pay
            Order Date
            Payment Method
            Due Today
            Flutterwave
              Subscription Successful

              Congratulations! You have successfully activated Boomplay 1 Month Premium.

              Now you have access to all the features of Boomplay App.
              Payment Failed

              Please check your balance and then try again.

              You'll lose your subscription if we don't have a working payment method for your account, so please check your payment details.
              Need help? Contact Boomplay Subscription Support.
              Payment Processing...
              10 s

              Payment is being processed by . Please wait while the order is being comfirmed.

              Payment Processing
              Your order is processing, and it may take up to a few days for the service provider to handle your payment. Please kindly stay tuned and check your order status in ‘User Center’.
              About Order Status