Loading...

Download
  • Genre:Afrobeats
  • Year of Release:2007

Lyrics

Amekoma ft. Q Chief - Mh Temba

...

chorous

Amekoma amekoma amekoma

Amekoma amekooma amekoma

Alidhani poa poa kumbe sio poa aaah side mnyamwezi

Alidhani poa poa kumbe so poa aaah side mnyamwezi


Verse 1

Anaitwa side said mnyamwezi mtoto wa mbezi

Mtu wakulipuka pamba ile kishenzi

Anamiliki prado colora pamoja na benzi

Ni kijana mcheshi mtanashati ushauri huwa hataki

Matumizi yake kwa siku yanazid laki

mimi namsimulia story yake sababu nimekua naye huyu nimesoma naye huyu hata sasa nishagombana nae

Wazazi walimshauri huyu akawana kiburi

Hakuwa na malengo wala dira kama taila

Ni mwongo mtoa fix wa kuaribu mabinti

Hana mapenzi ya kweli analaghai wakina dada

Mwishowe aliwatelekeza bila kutoa msaada

Alikuwa mpenda sifa demu wake wa kwanza alikuwa Latifa

Penzi halikudumu sana miezi kadhaa wakaachana

Hii ilikuwa furaha kwake kashamaliza haja zake yule akaenda zake

Akaja akang'oa mwingine alikuwa ni demu wa rafiki yake

Yeye hatambui hilo anahamishia tu kwake

Na juzi kafumwa guest na mtoto wa dada yake

Tabia yake na mambo yake wengi hawakuipenda

Masela mtaani washapanga dili wampige mawe

Wazee wamekaa vikao wanatamani wamuue

Huyu jamaa wanamwita Kiwembe hywa abakizi demu

Mtaani alimpaka razia tukajua anamchumbia

Kila siku anaye kwenye gari wanakula raha za dunia

Alimgharamia mpaka tukajua anaona

Kumbe maisha ya yule binti anaenda kuyatia doa

Razia atake nini asipewe chochote kisichelewe utasikia nataka gari

Tulia ntakupa nataka simu usihofu ntakupa

Hii tabia sijui amerithi au unelogezewa

Anayoyafanya jamani nahisi ametumwa na shetani

kashagombana na rafiki zake kisa wanawake

Side huyo


chorous

Amekoma amekoma amekoma

Amekoma amekoma amekoma

Alidhani poa poa kumbe so poa aaah side mnyamwezi

Alidhani poa poa kumbe so poa aaah side mnyamwezi


verse 2

Side huyo side huyo mnyamwezi huyu hapa tena

Akishamaliza anatema aliendelea na tabia yake ili afurahishe moyo wake

Alishapata kesi ya kumtorosha mwanafunzi

Na hivi juzi juzi badala ya kung'oa demu kang'oa shoga

Akaenda kula kiboga bila woga

Kwa tabia yake ya kishenzi akashindwa kuishi mbezi

Akaja akahamia Chang'ombe akapata demu Shombe Shombe anakunywa pombe

Alimlea vizuri akamhonga mpaka gari kwao akatoa mahali

Ni starehe juu ya starehe wanakula raha mazee

Kwa kuwa alikuwa nao wengi hakujua amchukue amuoe yupi

Alhamisi ladies is free kama kawaida billcanas

Akaenda akang'oa mlupo alikuwa na rafiki zake akawatelekeza wenzake

Eti kisa demu ndio unawatelekeza masela

Aliondoka na yule demu akaenda kujipunzisha

Kumbe demu si demu demu mwenyewe anatisha popote utakapo mfikisha lazima atalianzisha

Vimbwanga vilipomkuta ilibidi side adate

Wamefika guest ndani picha linaanza

Demu nini... anataka kumvua kimini

Demu kaanguka chini anataka kumsogelea demu kapotea

Anataka kumkumbatia demu kageuka kawa ngamia

Side anaanza kulia anatafuta njia ya kukimbilia

Binti anaanza kubadilika sura za ajabu ajabu

Mara ratifa mara razia mara stella eh eh mara akageuka Rashidi

Ikabidi side atoke nduki guest uchi

Huku anapiga kelele kama mwizi au chizi

Walinzi wamemkosakosa walijua mwizi yuko uchi wa mnyama watu angali wanamtazama

Anaita mamamama kimefika kiama ikabidi waungwana wamsitiri kwa kumpa nguo

Anaapa amekoma Chang'ombe nzima anaona noma

Wiki nzima hii hajatoka nje anaona aibu kwa yaliyo msibu

Side huyo side huyo mnyamwezi

Yeah yeah


Chorous

Amekoma amekoma amekoma

Amekoma amekoma amekoma

Alidhani poa poa kumbe so poa aaah side mnyamwezi

Alidhani poa poa kumbe so poa aaah side mnyamwezi


Q-chief

Anauza sura masaki anaishi geto Magomeni

Choo cha kulenga ugali tembele nyumba ya makuti side mnyamwezi

Wanaume walimwambia lakini wapi mchizi hakutaka kusikia kila tulichomwambia lakini wapi mchizi hataki kusikia

Jibu lake aaah wapi kwa machizi aaah wapi kwa masela aaah wapi


Chorous

Amekoma amekoma amekoma

Amekoma amekoma amekoma

Alidhani poa poa kumbe so poa aaah side mnyamwezi

Alidhani poa poa kumbe so poa aaah side mnyamwezi

Similar Songs

+

      -   or   -

      -   or   -

      NG +234

          Please Select A Playlist

          Add New Playlist

          Share on

          Embed: Love & Light EP

          Custom Size :

          • Default
          • Desktop(300*600)
          • Mobile(300*250)

          Type :

          • HTML/HTML5 (WordPress Supported)
          Get Boomplay Premium
          for
          Payment Method
          Pay With
            Review and pay
            Order Date
            Payment Method
            Due Today
            Flutterwave
              Subscription Successful

              Congratulations! You have successfully activated Boomplay 1 Month Premium.

              Now you have access to all the features of Boomplay App.
              Payment Failed

              Please check your balance and then try again.

              You'll lose your subscription if we don't have a working payment method for your account, so please check your payment details.
              Need help? Contact Boomplay Subscription Support.
              Payment Processing...
              10 s

              Payment is being processed by . Please wait while the order is being comfirmed.

              Payment Processing
              Your order is processing, and it may take up to a few days for the service provider to handle your payment. Please kindly stay tuned and check your order status in ‘User Center’.
              About Order Status