Loading...

Download
  • Genre:Hip Hop & Rap
  • Year of Release:2023

Lyrics

Nipeni maua yangu ft. Abiud - Roma Mkatoliki

...

Wamemchokoza Bea!

Tumekumisi Roma

Rudi nyumbani Roma

Uwatetee wanyonge ndugu zako

Uwakumbushe viongozi

Sasa sijui nianzie wapi kifuani nimebeba mengi

Na sitotenda haki nisiposema hiki sipendi

Hiki napenda kile sitaki mambo ya kishenzi

Tanzania haijaezekwa bati na wamekula pesa ya ujenzi

Yaani nchi wanaifanya mti mjenzi anauona mbao

Ndege ataona makazi mkulima ataona mazao

Mganga atauona dawa na mpishi atauona kuni

Ataemiliki mwenye power sisi atatusagia kunguni

Na ukisema hawatufai wanakuumiza uwe mpole

Yaani wanaangua papai kwa kutumia gobole

Wanatumia nguvu kubwa kwenye mambo madogo

Jeshi gani mpaka leo mmeshindwa kumjua kigogo

Tukiongelea kutekwa eti tunarudia ajenda

Hamjibu mnakwepa mbona mama anarudia kilemba

Nchi gani raia akihoji mnasema anakosoa

Na akikosoa anatukana serikali hii sio poa

Haya basi tuseme mko sawa na mna nia nzuri na sisi

Mbona vyuma vimekaza halafu mama anaificha grease

Mara mkapandisha tozo kampeni mkono hatuwaungi

Si tulihoji mkajibu kwa dharau tuhamie Burundi

Tatizo mkishaapishwa tu mnawaza uchaguzi ujao

Hamuwazi njia mbadala ya kumlinda mkulima na mazao

Sasa Iringa si tuna msitu halafu tuspick twaagiza China

Manaake hapo kwanza ncheke yaani Bongo kikubwa uzima tu

Sa mnatuambia tujiajiri mbona nyinyi hamkujiajiri Okay nikupe boda yangu kisha we unipe uwaziri

Nikukabidhi vyeti vyangu hangaika navyo mwezi mmoja

Niko pale nakungoja uje tuongee lugha moja

Mi sio CCM sio CHADEMA hili niliweke wazi

Ila ukiweka CCM na Andazi nitachagua Andazi

Simuamini mtawala na mpinzani simsadiki

Maana wanaendelea kukatika huku DJ kauzima mziki

Na inaniuma kuona kijana msomi wa degree tatu

Nashindwa kumpa ajira sasa anauza nyanya karatu

Sasa sijui mtaniua nikimshikia mama shilingi

Maana hata inyeshe mvua mnasema anaupiga mwingi

Na ninamkubali na nitamng’ata sikio kama hajui

Wanaomkosoa ndo wanampenda wanaomsifia ndo maadui

Ili wapate teuzi ndo wanamlamba miguu

Wakimpamba hawamsaidii Amiri Jeshi Mkuu

TUNAKUPENDA ROMA

TUNAKUMISS ROMA

RUDI NYUMBANI ROMA

UTUSEMEE

TUNAKUPENDA BABA

TUNAKUMISS MWANA

TUNAKUKUMBUKA SANA

Hivi hamjasikia tetesi kuwa remote iko msoga

Si huku mageng imedoda magogoni imenona

Watu tatu ndani ya track moja wamekalia kigoda

Ngolo Kante anampa Mbappe cross anafunga Pogba

Hii nchi ina wenye nchi walanchi na wananchi

Na kuendelea kuwachagua ni kwenda na mchanga mbichi

Tuwajaribu na wapinzani watawala si wameshapata

Ugoro umewaingia puani sasa ona wanapiga chafya

Wanatumia dollar kubaki kuongoza dollar

Watawafunga watapora wataua watahonga vijora

Karatasi tunaibiwa za kura kwenye sanduku

Kwa hiyo mnatuonyesha ziwa huku mmeziziba chuchu

Okay kura ziko 300 na kuna watu mia kwa jimbo

Na kituoni hakukua na watu halafu wameshinda kwa kishindo

Sa kama Askofu mfufua watu ameiba kura za mpinzani

Je atashindwa kuiba sadaka za waumini kanisani?

Hii ni gani mchungaji akitaka gari twamchangia

Muumini akitaka gari anaombewa tunamsalia

Sa mchungaji tusimpe pesa tumuombee na yeye pia

Tukae pale tusubiri miujiza ya wagalatia

Wabunge wengi mlishinda kwa hisani ya mwendazake

Mkipatacho muende Chato mkumbuke hata ndugu zake

Jimbo hili haliendelei cause mmemchagua mpinzani

Haya sasa mmeshinda kote fauluni huo mtihani

Turuhusu siasa za amani turudi zile enzi zetu

Uchaguzi sio siku moja ni mchakato wa muda mrefu

Mikutano ya nje na ndani ndo tunaimarisha chama

Daily mtulishe majani halafu sikukuu mtupe shawarma

Keki ya taifa ni kubwa tuache siasa za risasi

Mnawaonea wakishika dola watalipa kisasi

Tulipotoka ni mbali siasa za mwendazake

Msirudi msilale chali huku mnatutemea mate

Na BASATA msikie hili msije fungia huu wimbo

Kichwa kisicho na akili ni mzigo kwa shingo

Sawa tulinde maadili ila tusiue wabunifu

Mtupende tunaokosoa kama mpendavyo wanaosifu

Wengine wamekuwa viongozi na mliwaona tu marapa

Hiphop ni mkombozi na sauti isiyo na mipaka

Ushauliza kwanini bega lipo karibu na kwapa

Usiondoke baki hapa usikie verse inayofuata

(REPEAT CHORUS)

More Lyrics from Roma Mkatoliki Songs

Similar Songs

+

      -   or   -

      -   or   -

      NG +234

          Please Select A Playlist

          Add New Playlist

          Share on

          Embed: Love & Light EP

          Custom Size :

          • Default
          • Desktop(300*600)
          • Mobile(300*250)

          Type :

          • HTML/HTML5 (WordPress Supported)
          Get Boomplay Premium
          for
          Payment Method
          Pay With
            Review and pay
            Order Date
            Payment Method
            Due Today
            Flutterwave
              Subscription Successful

              Congratulations! You have successfully activated Boomplay 1 Month Premium.

              Now you have access to all the features of Boomplay App.
              Payment Failed

              Please check your balance and then try again.

              You'll lose your subscription if we don't have a working payment method for your account, so please check your payment details.
              Need help? Contact Boomplay Subscription Support.
              Payment Processing...
              10 s

              Payment is being processed by . Please wait while the order is being comfirmed.

              Payment Processing
              Your order is processing, and it may take up to a few days for the service provider to handle your payment. Please kindly stay tuned and check your order status in ‘User Center’.
              About Order Status