Yesu ni furaha yangu Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2023
Lyrics
Yesu ni furaha yangu - Papi Clever & Dorcas
...
1.Yesu ni furaha yangu, amejaa pendo kweli.
Anaweza kusimika kila mwenye udhaifu.
( Ananipa ujasiri, nguvu, raha na faraja.Hata nikionja kufa, Yesu ni mchunga wangu)×2
2.Nimefungwa na Mwokozi kwa kifungu cha upendo.
Hata kufa hakuwezi kunitenga naye Yesu.
(Mimi wake siku zote, ninataka kumtii. Kwa neema nimepona, nisitumikie dhambi)×2
3.Kwa mikono ya upendo ninakumbatiwa naye.
Sitaweza kutafsiri pendo lake kubwa kwangu.
(Napokea nguvu yake, yanijaza moyo wangu, Yesu ananiongoza katika safari yangu)×2
(Yesu ananiongoza,katika safari yangu)×2