Sijafika Lyrics
- Genre:Afrobeats
- Year of Release:2022
Lyrics
Sijafika - KO Kenya
...
yeee oooh oo
k.o
muumba hivi nimejaliwa ati mwengine anaingiziwa
ooh binadamu niwaambieje hawa
kodi nyumbani ninadaiwa
ume titia inanijua
hasa ndo nilikameje haya
kwenye mziki niendelee
ama nisite
nguzo ipi niegemee
nipumuzikee
hivi ninapalilia shamba langu
ama wengine ndio watavuna
maana vitani kuna wenzangu
ila silaha yoyote sina
nimechacha kote wananifahamu
machozi nafuta wengi wakitabasamu
bado bado bado
ningali natembea na niko karibu kuanguka
bado bado bado
mwendo ni wa kuchechemea
ila sidhani nitafika
(instruments)
wanangu wa karibu wanasafiri
haya majaribu yananikabili
na ni zangu aibu hazisitiri
ama nikoaje
mavumbi kwa majivu
umezikwa mwili
hunishuki wivu unayatabiri
navuna mbichi mbivu nina maswali
itakuaje
japo mziki kwangu kipaji
ila ndio njia ya usemaji
langu limeingia maji
naweka wazi
nakabiliwa na mahitaji
familia ndugu wazazi
nakosa nguvu kupiga kazi
nisarakasi
nimechacha kote wananifahamu machozi nafuta
wengi wakitabasamu
bado bado bado
ningali natembea na niko karibu kuanguka
bado bado bado
mwendo ni wa kuchechemea
ila sidhani nitafika
aiyoyo
aiyoo