NURU YA ULIMWENGU Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2021
Lyrics
Nuru ya ulimwengu, chumvi ya dunia.
mimi nawe tumeokolewa tuangaze dunia
Nuru yake Yesu.
Kwa neema ya Mungu, tumestahilishwa
Mimi na wewe tumepewa dhamana
Mawakili wa siri, zake baba Mungu.
Tena tu mashahidi wa wema na uzuri,
wake Mungu tumepewa baraka,
ziwavute wengine waje kwake Yesu.
Nuru ya ulimwengu, chumvi ya dunia.
Mimi nawe tumeokolewa tuangaze dunia
Nuru yake Yesu.
Uwepo wetu ni wa Thamani,
katika uso wa dunia.
Nafasi yetu ni ya muhimu,
katika uso wa dunia.
Mwili wa kristo kanisa la Mungu
(tuungane)
kuangaza dunia watu wayaone
( matendo yetu)
tuwe wa moja twende kwa pamoja
( tuungane)
kungaza dunia watu wayaonee
(matendo yetu)