HAZINA YANGU Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2021
Lyrics
Nimewekeza hazina yangu juu mbinguni,
Nimewekeza kwa Mungu wangu.
Nimeyatoa maisha yangu niwe dhabihu,
Nimejitoa kwa Mungu wangu.
Mambo ya dunia ni ya kitambo tu,
Ya haribika Tena yapita.
Hakita bakia kitu kwa dunia,
Vya haribika tena vya pita.
Nimewekeza hazina yangu juu mbinguni,
Nimewekeza kwa Mungu wangu.
Nimeyatoa maisha yangu niwe dhabihu,
Nimejitoa kwa Mungu wangu.
Mimi nita-jisifia nini cha ulimwengu,
Hata kifanye nimkosee Mungu.
Vyote ni kwa mapenzi ya Mungu,Si kwa nguvu zangu
Nataka nifae mbele za Mungu.
Kwake Mungu hakuna nondo madumadu na parare,
Mimi nataka nifae mbele za Mungu.
Huko iliko hazina yangu, Ndiko uliko moyo wangu,
Mimi nataka nifae mbele za Mungu.
Wekeni hazina mbinguni,
Haita pungua akiba yenu Mbinguni kwa Baba
Jifanyieni mifuko, isiyo chakaa kabisa,
Mbinguni kwa Baba.