- Genre:Gospel
- Year of Release:2023
Lyrics
Heri asiye fuata shauri la waovu,
Wasio shiriki njia za wenye dhambi,
Wala kujumuika na wenye dharau,
Bali Hufurahia sheria yake mungu,
Huyo ni kama mti kando ya kijito,
Unaoza matunda kwa wakati wake,
Na majani yake huwa hayanyauki,
Kila afanyalo hakika lafanikiwa.
Itakuwa furaha kwa waumini,
Waliofuata sheria yake mwenyezi mungu,
Nafsi zao,hazikushiba mzaha,
wa wenye raha na dharau ya wenye kiburi,
Na watakaa kwa meza ile ya kifalme,
Wao ni wana wa mbingu.
Ingawa bwana yupo juu yu macho,
Aona mnyenyekevu wa moyo tokea mbali,
Pia amwona mwenye majivuno,
Kwa upendo ampa nafasi ya pili,
Tengeneza mapito uwe mti wa kijito,
Wenye mazao bora.
Itakuwa furaha kwa waumini,
Waliofuata sheria yake mwenyezi mungu,
Nafsi zao,hazikushiba mzaha,
wa wenye raha na dharau ya wenye kiburi,
Na watakaa kwa meza ile ya kifalme,
Wao ni wana wa mbingu.