Sadaka Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2023
Lyrics
Je moyo wako upo safi
Unapotoa sadaka zako kwa mungu
Je wanyenyekea na kuweka mbali kiburi
Utii kwake Mungu muumba wako
Je waendana na matoleo yako
Ni wazi wajua bwana mungu auchunguza moyo
Utii kwake Mungu wetu ni zaidi ya sadako zetu
Kwani nchi na vyote vijazavyo
Ni mali ya mungu
Bwana asema utii kwake ni bora kuliko dhabihu zetu zisizo kamili
Tumtii mungututoe kwa ukamilifu
Kumbuka dhambi inatutengana uso wa mungu
Hivyo sadaka zetu si kitu mbele za mungu
Ikiwa tu wa dhambi tuje mbele za mungu
Kwa unyenyekevu na mioyo ya kupondeka
Ndipo sadaka zetuzitakubalika mbele za mungu
Utii kwake Mungu wetu ni zaidi ya sadako zetu
Kwani nchi na vyote vijazavyo
Ni mali ya mungu
Bwana asema utii kwake ni bora kuliko dhabihu zetu zisizo kamili
Tumtii mungututoe kwa ukamilifu