Ex Boyfriend Lyrics
- Genre:Bongo Flava
- Year of Release:2021
Lyrics
Ex Boyfriend - Rayvanny
...
Leo nakula kwa macho, nguvu ya kusema sina. Maneno ya mipasho na jeuri vimeshazima. Nilishafuta number zako, nikachoma picha zako,sikujali ulivyolia,mbele ya mashoga zako, nikasema uende zako,nguo nikakutupia. Na zaidi, uliuguza vidonda kwa vipigo, manyanyaso kila siku. kwa mawazo ukakonda, niko busy kucheat nafungua zipu.
ulinibembeleza, nikakubeza, unanuka na nikakutelekeza. macho makengeza, miguu ya pweza, kuwa nawe nikasema niliteleza. Leo unapendeza wamekutengeneza, wanaume wenye mali wenye fedha. sasa unajiweza, siwezi kujikweza, najutia nafasi kuipoteza.
leo aibu yangu, ex boyfriend, ex boyfriend, ex boyfriend...siiti tena honey, baby, jina langu limekuwa ex boyfriend, ex boyfriend, ex boyfriend , sikujua kumbe tabu peke yangu naugua.
nawaza nilifeli wapi kusema sikutaki,sura ya baba na kitambi cha makapi, sa una mtanashati, bitozi tena smart, mtu wa gym tena ana sixpark. mi nipo juu ya bati, sina mikakati, ghetto mwendo chai na chapati, we ushahama mburahati, una nyumba masaki, mnachoma nyama kila siku party. ushanipiga mikuki aah, insta mi sifurukuti aah, mambo ya gauni suti aah, mkipiga photo shoot aah. mapenzi hayana commando, mwenzako inaniuma roho, natamani nikuite njoo, turudi kama before, kumbe shape ilijificha kwenye dera, hizo skin jeans mama zinakera, utaniletea card kwenye machela, siku akikuvalisha shera.
na ulinibembeleza, nikakubeza, unanuka na nikakutelekeza, macho makengeza, miguu ya pweza, kuwa nawe nikasema niliteleza. leo unapendeza wamekutengeneza, wanaume wenye mali wenye fedha, sasa unajiweza na sio unajikweza, najutia nafasi kuipoteza. leo aibu yangu, ex boyfriend, ex boyfriend, ex boyfriend, siiti tena honey, baby, jina langu limekuwa ex boyfriend, ex boyfriend, ex boyfriend, sikujua kumbe tabu peke yangu naugua.