Nitabibu Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2022
Lyrics
Nitabibu - Beatrice Mwaipaja
...
Ni tabibu wa karibu,
Tabibu wa ajabu,
Na rehema za daima,
Ni dawa yake njema.
Imbeni malaika,
Sifa za Yesu bwana,
Pweke limetukuka,
Jina lake yesu.
Hatufai kua hai,
Wala hatutumai,
Ila yeye ndiye kweli,
Atupimuzishaye.
Imbeni malaika,
Sifa za Yesu bwana,
Pweke limetukuka,
Jina lake yesu
Dhambi pia na hatia
Ametuchukulia
Twendeni na amani
Hata kwake mbinguni
Imbeni malaika,
Sifa za Yesu bwana,
Pweke limetukuka,
Jina lake yesu
Huliona tamu jina
La Yesu Kristo bwana
Yuna sifa mwenye Kufa
Asishindwe na Kufa
Imbeni malaika,
Sifa za Yesu bwana,
Pweke limetukuka,
Jina lake yesu
Kila mume asimame
Sifa zake zivume
Wanawake na washike
Kusifu jina lake
Imbeni malaika,
Sifa za Yesu bwana,
Pweke limetukuka,
Jina lake yesu
Na vijana wote tena
Wampendao sana
Waje kwake wawe wake
Kwa utumishi wake
Imbeni malaika,
Sifa za Yesu bwana,
Pweke limetukuka,
Jina lake yesu