Kwaru Lyrics
- Genre:Bongo Flava
- Year of Release:2021
Lyrics
Kwaru - Zuchu
...
oooh ooh ooh ooh oooh
Roho ingekuwa na macho ngejionea,
Moyo haufanyi kificho ukigotea,
Mimi kipi nisonacho ngeongea
Mwili wangu rochorocho nanyongonyea
chungu nilichopika wamepakua wenzangu,
Huruma napukutishwa wamechukua donge langu,
Na kitabu chetu cha mapenzi kurasa umechanachana,
Hazisomeki tena tenzi zimepoteza maana,
Mpofu moyo wangu ulishindwa ona hukuandikwa wa kwangu,
limenikapa nalitema,
Kwaru kwa kwaru kwaru
kachukua kisoda anaukwarua
kwaru kwa kwaru kwaru
Moyo wangu unaumia
kwaru kwa kwaru kwaru
Ye kwa nguvu anaukwarua
kwaru kwa kwaru kwaru
Jamani moyo wangu unaumia
Eeh langu tatizo nachuna najimaliza,
Mi nakesha kumuwaza naweweseka lake jina(ooh jina)
Ooh basi kwa unyonge najikaza niache kulia,
Maana kwake bahati sina (ooh sina)
Maumivu ameipora furaha yangu (oooh amekwenda nayo)
Na zangu mbivu zimeniozea,
Hasara kwangu oooh yatapita hayo.
Mpofu moyo wangu ulishindwa ona hukuandikwa wa kwangu,
limenikapa nalitema,
Kwaru kwa kwaru
kachukua kisoda anaukwarua
kwaru kwa kwaru kwaru
Moyo wangu unaumia
kwaru kwa kwaru kwaru
Ye kwa nguvu anaukwarua
kwaru kwa kwaru kwaru
Jamani moyo wangu unaumia