Kilio Lyrics
- Genre:Bongo Flava
- Year of Release:2018
Lyrics
Kilio - Lava Lava
...
Mmmmh, mmmmh
Hali yangu mbaya, hanifikirii akipata muda, akipata muda
Moyo ameshaugawa, pakacha penzi linavuja, limeshavuja
Mwenzie napagawa, nahisi uchizi, na network haisomi
Mmmmh
Anayofanya si sawa, nakosa usingizi, mwilini washwa na vichomi
Iiiiiih
Mwamniee, kutwa mateso nasurubiwa
Mwenzieee, yatima mapenzi mwana mkiwa
Ooh mie, mapenzi ugonjwa nimezidiwa
Mieeh, kwengine sioni kunitibiaa
Uuh
(Kilioo, Kilioo) kilio na penzi langu
(Kilioo kilio) huruma haanaa
(Kilioo kilio) ya rabbi Mola wangu
(Kilioo kilio) japo simama
Mmmmmh
Ye ndo barafu, niliyemlia yamini
Pemba karafuu, marashi yangu mwilini
Utamu wa dafu, mbona ameutia kwinini
Amenchezea rafu, penzi amelikafini
Eeeh
Ye anajivinjari mwenzake nadoda, napata tu habari anagawa uroda
Tetemeko moyo kupenda uoga, najiepusha mbali kukwepa vioja
Mwamniee, kutwa mateso nasurubiwa
Ooh miee, yatima mapenzi mwana mkiwa
Ooh miee, mapenzi ugonjwa nimezidiwa
Miee, kwengine sioni kunitibiaa
Uuh
(kilioo kilio) kilio na penzi langu
(kilioo kilio) huruma hana
(kilioo kilio) ya rabbi Mola wangu
(kilioo kilio) japo simama
Moyo wangu bado (mtekemteke )
Asinikondeshe
Mwenzake bado (mtekemteke )
Asinizeeshe
MI mdogo bado (mtekemteke)
Asinikomaze roho
Moyo bado (mtekemteke)
Iiiiiiih