Mlemavu Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2021
This song is not currently available in your region.
Lyrics
Mlemavu - Dizasta Vina
...
. . .
Haujui Wimbo uliobora Dhahiri
Haujui Ushairi au mstari ukaukariri
Haujui Giza haujui baridi au Mbu walonigasi wakati Nakusubiri
Haujui kupenda moyo wako hewa
Wote tunajifunza ila mwenzangu Umechelewa
Kaa kimya hauna hata haki ya kusema
Upuuzi unaoufanya si ushujaa ni ukilema
Natamani upate kimista pengine kikuumize kama ulivoumiza Wengine
Unaumwa mama hata Kwa matibabu hautapona
Sio dhahabu naijua dhahabu nikiona
Kuvimba kwako kamwe hakutavunja Miamba
Ipo siku utajua kuwa kulinda si Afya
Utatafuta upendo utanizikuta Siasa utaelewa inavouma pindi unavofanywa wa ziada
Kutojibu jumbe za Simu sijui ndo kula njama
Kudanganya mahali ulipo umeshavuka zama
Huu ushenzi ni uzamani upo nyuma Mama unapodhani ni Ujanja nakuonea Huruma sana
Eti "Queen" Queen hawezi choropoa Mimba
Ungekufa Kwa ngoma kinachokuokoa Kinga
Unajirusha sana itakukatikia kamba utazubaa na Uzee utakukutia njia panda
Unanuka sana unanitia kichefuchefu nimepoteza muda umenirudisha nyuma Step
Tunda huishia tumboni likiinzia kwenye mbegu Mama nimeshindwa Sasa nawaachia walimwengu
Nakupigia Simu hupokei nakutext ku-reply Unavex
Kwakuwa we ni mzuri unatafutwa na wengi Ivo unajiona keki
Mlemavu
Kutokujua kupenda si Ujanja ni ULEMAVU
Kwenye simu ulivonisave ni Fundibomba
Ndo nkajua inavokata stimu kujikosha
Nywele ulichukua ukaichezea na Kuitupa
Utaenda mbali siku utarudi kuitafuta na hautaiona tena
Sas utaweweseka Utapojua uzuri hauzuii Kuzeeka
Utakufa hautaacha alama Wala ngao kama urithi zaidi ya picha chafu kwenye Mitandao
Namuonea Huruma bwanaako wa sasa si Uongo uko aliko anahisi ameliokota Dodo
Kumbe chizi ulieshindikana milembe na kama unajiona mzuri sana Jipende
Mchoyo we Mama unamtima wa aina gani, Utaacha lini izo Bima za Wahisani
Moyo wako haujui kupenda asilani haujawahi hata kulala na picha Kitandani
Haujawahi kuona watu wakighairi masomo
Wanazijua sheria lakini bado wanavunja sababu ya kupenda wanakaidi maonyo
Haujui Chochote zaidi ya hizo style za Ngono
Rafiki yako Mage tumetoka Kumzika wenye akili tunajifunza kwa huu msiba
Lakini Wasio na haya hawaijui kuwa hakuna tuzo ya Umalaya mwanaizaya Pumzika
Ulinibeba ili uje kuntupa nlijiachia nimeumia Sasa nimejifunza
Siwezi sema hautapata bwana kama Mimi tupo wengi lakini Utankumbuka naamini
Nakupigia Simu hupokei nakutext ku-reply Unavex
Kwakuwa we ni mzuri unatafutwa na wengi Ivo unajiona keki
Mlemavu
Kutokujua kupenda si Ujanja ni ULEMAVU
...
Nakupigia Simu hupokei nakutext ku-reply Unavex
Kwakuwa we ni mzuri unatafutwa na wengi Ivo unajiona keki
Mlemavu
Kutokujua kupenda si Ujanja ni ULEMAVU
..
(Instrument)
...
(Lyrics by AT Man Don)
..
BINGO BEATS (Prod:Sign)