Loading...

Download
  • Genre:Hip Hop & Rap
  • Year of Release:2022

Lyrics

Shahidi - Dizasta Vina

...

Shahidi

Ah

Nilipanda kwenye jukwaa, watu walinishangaa,

Unadhifu wa meli haukufanana na nilivyovaa

Kabla sijatoa salamu, walipoteza hamu

ya kuburudika wengine wakaanza kusambaa

Nilikuwa na nywele nyingi zilionyesha pia siku ni nyingi tangu mara ya mwisho ziwekwe maji,

Wale Matajiri waliosheheni kwenye viti walicheka wakihisi mi’ chizi au mchekeshaji

Walio karibu pia wakaanza kun’tunza pesa

Na walio mbali walijaribu kurusha fedha,

Kwa yote niliyowaeleza hakuna alieyaweka kichwani

Wote walihisi kuwa nataka kuchekesha

Walinitemea shombo kwa kejeli

Wengine walihisi nalianzisha zogo kwenye meli

Mwonekano haukuyabeba maneno yangu

Hawakuamini niliposema kuwa chombo kina mushkeli

Niliwaeleza kuwa kule ndani kuna tundu dogo

Linapitisha maji linazamisha chombo

Waliendelea kujadili siasa na vibonzo

Hakuna aliyejadili kuhusu roho

Za wasakatonge wanyonge wasafiri daraja la tatu

Hawakulipa pesa nyingi ila walikuwa ni watu

Maji yalianza kuingia vyumbani mwao

iliwekwa mipaka hivyo taarifa hazikufika katu

Nilienda mpaka chumba cha sauti

Nitoe tangazo kabla hatujakumbwa na mauti

Mtoa sauti aliwataja matajiri

akiwapa sifa majina makubwa na saluti

Niliwaambia wekeni glasi chini mtege masikio

Hizo kelele mnazosikia si sherehe ni vilio

Wakasema nimedata nataka kuanzisha vagi

Ilionyesha wazi hawakuona mbeleni tishio

Hata kwenye vyumba vya wasomi maarufu

Vyeti walihodhi maradufu

Niliwahoji kuhusu ubovu wa meli wengi

waliujua ubovu lakini walisema haiwahusu

Naapa haki nilienda kote..

Nilihamaki kuona wote wamepewa cocktail

walikunywa na kula bata, walikunywa hata

mziki waliruka mpaka mafundi walilewa pombe

Wakasema huyu ni mjinga hajielewi

Kisha wakanituhumu mi’ ni mlevi wakati

Wamelewa wao, wakanipa matusi ya kienyeji

Hawakutaka kusikiliza hata semi

Nilimwona nahodha nikahisi nimeipata nafuu

Alikua kando ya mrembo fulani hivi daraja la juu

Gauni refu mwili mzima amepakaza tatuu

Aliponiona aliendelea kuikata tamboo

Kweli starehe inaweza kukufanya hauoni

Kukufanya hauoni

Kwani licha ya kujua nipo hapo kutoa

taarifa nahonda na mrembo waliendelea kushikana maungoni

Nahodha akaipaza miguno, akinipuuza

Mrembo naye akafata mkumbo,

Nahodha akachukua chupa akakata mafundo

Wakaendelea kupapasana mifumo


Ya viungo vyao vya uzazi walikuwa radhi kuzika shift

Hawakusikia chochote nilichosema

Nakumbuka mrembo alidiriki kuniita mwizi

Nikafatwa nikaja kupigwa na walinzi

Wenzangu waliogundua ubovu wa chombo walihofu

Wakaamka wakawahi kubeba vyombo vya wokovu

Walikaa kimya kwa sababu tu ya ubinafsi

Mi’ nikabaki ili niziokoe roho za wachovu

Ilikuwa bahati mbaya hakuna aliyesadiki,

Mshereheshaji akaongeza sauti kubwa ya mziki

Kiasi sauti yangu ikaanza kuwa haisikiki

Walinzi walitumwa wanidhibiti

Nilifungwa kwenye chumba chenye giza chini nisihame

Nikachapwa mijeledi thelathini na minane

Nikapambana nikatoroka na mtumbwi kwenda kando

Usalama wangu ulianza hapo

Nilishuhudia kila inchi ya ile meli ikizama

Roho za kila mkwezi zikihama

kutoka uhai kwenda kifo, sikufurahi kuona hivyo

Ila sikuwa na jambo ningeweza ‘fanya

Wakati walokole wakiombea kupona

Tajiri na maskini waligombea maboya

Wanazi walionicheka wakasema mi’ ni zuzu

walikufa wote hata walionisema kinoma

Ahadi ya maisha mapya ilisemwa ila hakuna aliyekumbuka,

Pesa zilizagaa na hazikuguswa,

Hata wale waumini walioitamani mbingu

Na kuisifu, kumbe wote waliogopa kufa

Waliokuwa wanajikweza na ukubwa na ubosi mwingi

Yaliwaishia majivuni

Njia walizibuni, waliua mpaka wenza ili ‘kufosi kingi’

Kifo kiliwatia mbavuni

Walikufa wengi kama kuku kote walizagaa

Hata wanajeshi waliozijua ‘kareti’

‘Walidedi’ maana ujuzi wa mitutu haukufaa

Mbele ya kufa hakuna mwenye nguvu au shujaa

Nilishuhudia makafiri wakiungama

Masikini na Matajiri waligusana

Utu uliwatoka uasi ulisogea

Tofauti za kabila na rangi zilipotea

Watu wenye bendi na ‘tisheti’ zao za kijani

Walisahau kuwa nao pia wapo ndani

milango ilokuwa wazi yote ilijifunga

Walipiga kelele na mwisho walikufa maji

Washairi waswahili na tashtiti zao

Matajiri na masikini wote chini yao

Kwaya hazikutoa sauti ndimi zao

Walikufa wote mpaka mahujaji na dini zao

Wakati wa kufa hakuna dawa

Hakuna kiongozi hakuna chawa

Hakuna tofauti ya mali na milki zetu

Kwenye kufa hata wenye nacho na wasio nacho wanakuwa sawa

Hazikusaidia diplomasia za digitali

Asili ilihakikisha walosalia hawafiki mbali

Waliendelea kungoja msaada kwa tumaini

Mwisho wote walikufa sababu ya baridi kali

Walikufa makini sababu ya wapuuzi wachache

Walofanyia uzembe tangazo langu

Wamiliki walikula bima wakasingizia ajali

Ilihali meli ilizama mbele ya macho yangu… ah!

Viongozi hawakubebwa na vyeo vyao

maana wote walikuwa mbali na ridhaa

Niliona kofia za ufalme zikielea kando yao

Ila hakuna aliyekuwa hai kuzivaa

Niliwapa taarifa lakini wakanitwika maudhi

Waliishia kulia na hazikusikika sauti

Walipambana Mwisho yaliwafika mauti

Nilibaki hai kuziandika sarufi

Similar Songs

+

      -   or   -

      -   or   -

      NG +234

          Please Select A Playlist

          Add New Playlist

          Share on

          Embed: Love & Light EP

          Custom Size :

          • Default
          • Desktop(300*600)
          • Mobile(300*250)

          Type :

          • HTML/HTML5 (WordPress Supported)
          Get Boomplay Premium
          for
          Payment Method
          Pay With
            Review and pay
            Order Date
            Payment Method
            Due Today
            Flutterwave
              Subscription Successful

              Congratulations! You have successfully activated Boomplay 1 Month Premium.

              Now you have access to all the features of Boomplay App.
              Payment Failed

              Please check your balance and then try again.

              You'll lose your subscription if we don't have a working payment method for your account, so please check your payment details.
              Need help? Contact Boomplay Subscription Support.
              Payment Processing...
              10 s

              Payment is being processed by . Please wait while the order is being comfirmed.

              Payment Processing
              Your order is processing, and it may take up to a few days for the service provider to handle your payment. Please kindly stay tuned and check your order status in ‘User Center’.
              About Order Status