Loading...

Download
  • Genre:Hip Hop & Rap
  • Year of Release:2022

Lyrics

Hatia V - Dizasta Vina

...

Yeah

Nilimfahamu baba alikuwa jasiri

Aliondoa utando ulipodandia kuta

Alitoa nyoka makatili alipambana na

Majangiri walipovamia nyumba

Aliweka paa juu vichwa

Hatukuogopa baa la njaa tulishiba

Niliona wengine nguo za kuvaa zimechanika

Wakati kwetu nyuso ziling’aa migongo ilifunikwa

Radi ilipiga wala sikujali

Maana baba alikuwa Simba kwenye msitu mkali

Wapo waliozijua sifa zake japo

Mtaani halikuwika jina lake

Halikuandikwa bali

Waliona poa ilikuwa jukumu lake

Mwanaume jasho kutoa ndio hukumu yake

Ajali ya kisu iliondoa ngozi

Sikumwona akitoa machozi

Nilimwona kama Role model

Alikuwa shupavu hakuwa na roho ndogo

Mara chache alianguka ali-score zero

Alipambana upya kama war Hero mdogo mdogo.

Maisha yake yalikuwa ni adventure

Alikuwa ni Handyman Carpenter Painter

Alinijuza aliyoshuhudia kwa macho

Maana Aliisafiri dunia enzi zake kama Vasco

Alikuwa so gentle

Alimpenda mama kupita maelezo

Watu walijadili nini maana ya upendo

Waliunda dhana mi niliiona maana kwa vitendo

Huh

Ugonjwa uliingia mama aliugua maradhi

Homa ilivamia ghafla kupumua kazi

Baba ali-suffer Hospitali kadha wa kadha

Changamoto afya kupigania zikafungua jamvi huh

Hali ilileta mtiti

Hakuipata nafuu ugonjwa ulimweka kingi

Baba aliwapa Waganga wakuu pesa nyingi

Mixer kupelekwa majuu zinakoendeshwa ligi

Mama alilala hospitali miezi kumi na nane

Nyumbani miezi ilikuwa ni kama karne

Tulimzoea mama baba hakupagawa

Alisimama imara japo mambo hayakuwa sawa kamwe

Maisha yalibadilika tukabadilika pia

Familia ilipata shida ila baba aliisimamia

Ukubwa ulimshika majukumu yalishika njia

Yalimkaba shingo ila sikuwahi kusikia analia

Bahari ikichafuka inampima nahodha wa meli

Kama ataogopa kufa au ataongoza Kweli

Lakini si mawimbi samaki waliododosha meli

Bali ni rafiki wa karibu wa mama anaitwa Mary

Mary alimjali baba alimzidi Rose

Alimzidi Rahma alimzidi Shosi

Alimletea baba kadi aliniletea chopstick

Alifua nguo aliosha vyombo na alipika msosi

Aliingia mpaka chumbani kwa mdingi

Na udhaifu ukaanza yumbisha misingi

Mary alimshawishi baba baba akaingia kingi,

Kwa muda akamsahau mama akapitiwa akamsaliti ah

Hamu ya tendo ikawazidi maarifa

Kijakazi akazibeba taarifa

Miezi kadhaa baada ya mama kupona

Akasimulia yote aliyoyaona kama picha

Mama akatokwa na machozi

Baba akasota kwa magoti

Mbele yangu mi mwanae mbele ya wazee

Wakunga wa ndoa wenye busara waliobeba koki

Huh

Mama akapata mashoga wakali

Walitoka jangwa la Sahara na Kalahari

Wenye elimu za kutosha na ajenda kali

Wakamwambia talaka ukiomba utazipata mali

Mama akiwa na chembechembe za hasira

Akashawishiwa na wasomi wenye hira

kwa mbali wamezongwa na tamaa za ngawira

Akasahau kumsamehe kama ilivyosemwa mila

Mama akafungua jarada la talaka

Akaandaliwa Majeshi waliojipanga kwa karata

Baba aligoma kutoa talaka akiomba wamalizie nyumbani sio mahakamani na mama hakutaka

Mji ulifahamu kesi iling’ara

Yalipambwa magazeti mengi kwa nakala

Wanaume washenzi waliongea wapambe

Vijiwe vya uswazi waligawana pande ka masihara

Mzee hakukataa mwisho akakili kosa

Talaka ikaidhinishwa ndoa ikadondoka

Baba akapata uchungu likamshukia rungu

Kisha mama akaonyeshwa fungu akachota

Afya ya mama ya uchumi na mwili vikanawiri

Akawa Malkia mji ukatabiri

Baba akawa kama kifaranga kwenye mvua

Bado alimpenda mama na mama hakujua

Mama aliitwa Superwoman ama soja

Aliushinda usaliti aliushinda ugonjwa

Baba alimkosa mama kwa starehe ya usiku mmoja

Alimpenda mama hivyo kumpoteza maumivu tosha

Washiriki wa biashara walimweka kapuni

Akafukuzwa kazi asiharibu sura ya kampuni

Vikundi vya kina mama walisherekea kombe

Dingi aliipoteza kazi akaisogelea pombe

Hakuwa sawa kichwani aliishiwa Energy

Hakukuwa na counseling hakukuwa na Remedy

Zaidi Makala zilizoandikwa na Mafeminist

Pesa zilimwisha mtaani alifuga Enemies

Magazeti hayakuandika alivyokuwa hero

Yaliandika matusi yaliyomzidi kilo

Aliitwa Malaya shenzi katili

Mwanahizaya mwenye cheti cha ujangili

Na yakapiga millions

Hakukuwa na vyama vya wanaume kumtetea baba wakasema ana pepo la uzinzi

Ustawi wa maisha yetu ulipotea ghafla

Wanasheria wakala na pesa za ushindi

Aliumia peke yake Dunia ilimweka peku

Dhambi ilimwacha uchi hadharani

Alifanya mema zaidi ya kumi hayakutosha awe Yesu

Ila baya moja aliitwa Shetani Alizubaa

Alizubaa na akashikwa na madoa

Alikuwa shujaa ila alishindwa kujiokoa

Mwamba wa nyenzo ya katikati ulipoondoka

Ilimaanisha ni muda wa Safina kudondoka huh

Hazikusikika sifa zake njema

Machozi hayakusafisha jina lake tena

Haiba alizokuwa nazo hazikuvutia kamwe

msongo nao wa mawazo ukamvamia Mfalme

Aliandika barua ya hadithi yake

Akisema kilichomtesa sio dhiki yake

Bali ni uzito wa alichokifanya

Alijiua kando ya bahari uliokotwa mwili wake

Similar Songs

+

      -   or   -

      -   or   -

      NG +234

          Please Select A Playlist

          Add New Playlist

          Share on

          Embed: Love & Light EP

          Custom Size :

          • Default
          • Desktop(300*600)
          • Mobile(300*250)

          Type :

          • HTML/HTML5 (WordPress Supported)
          Get Boomplay Premium
          for
          Payment Method
          Pay With
            Review and pay
            Order Date
            Payment Method
            Due Today
            Flutterwave
              Subscription Successful

              Congratulations! You have successfully activated Boomplay 1 Month Premium.

              Now you have access to all the features of Boomplay App.
              Payment Failed

              Please check your balance and then try again.

              You'll lose your subscription if we don't have a working payment method for your account, so please check your payment details.
              Need help? Contact Boomplay Subscription Support.
              Payment Processing...
              10 s

              Payment is being processed by . Please wait while the order is being comfirmed.

              Payment Processing
              Your order is processing, and it may take up to a few days for the service provider to handle your payment. Please kindly stay tuned and check your order status in ‘User Center’.
              About Order Status