SAUTI YANGU Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2023
Lyrics
Sauti yangu (sauti yangu)
Ninaipaza (ninaipaza)
Nikuinue ewe uloniumba
Sauti yangu (sauti yangu)
Ninaipaza (ninaipaza)
Nikuinue ewe uloniumba
Ni mwamba wangu ni Mungu wangu
Jemedari wangu katika vita
Ye ndiye Baba kimbilio langu
Ye ndo uniokoa toka kwa shida
Mwokozi wangu anilindaye
Nitamuinua siku za maisha yangu yote Baba
Sauti yangu (sauti yangu)
Ninaipaza (ninaipaza)
Nikuinue ewe uloniumba
Sauti yangu (sauti yangu)
Ninaipaza (ninaipaza)
Nikuinue ewe uloniumba
Mhandisi mkuu Ye hunishangaza
Yote alotenda nani awezaye
Milima nayo alivyoiumba yasimama wima haitingiki
Tizama mito yatiririsha maji baharini na bahari halijai
Ni nani basi alo kaa Jehovah
Yeye pekee ndo astahili sifa Mungu wangu
Sauti yangu (sauti yangu)
Ninaipaza (ninaipaza)
Nikuinue ewe uloniumba
Sauti yangu (sauti yangu)
Ninaipaza (ninaipaza)
Nikuinue ewe uloniumba
Madakitari wanasayansi viongozi na wafalme wanamshangaa
Anavyoumba na kudumisha maisha ya watu hata wanyama
Yeye ajua siri za uumbaji
Yeye ndo pekee awezaye dumisha
Si utafiti wala elimu amewashinda
Astahili sifa Mungu wangu
Sauti yangu (sauti yangu)
Ninaipaza (ninaipaza)
Nikuinue ewe uloniumba
Sauti yangu (sauti yangu)
Ninaipaza (ninaipaza)
Nikuinue ewe uloniumba
Baba sauti yangu (sauti yangu)
Sauti yangu Mungu wangu (ninaipaza)
Haiyeyee naipaza kukuinua
Haiyee sauti hiyo (sauti yangu)
Sauti yangu Mungu wangu (ninaipaza)
Haiyee naipaza kukuinua
Haiyee sauti hiyo (sauti yangu)
Sauti yake Baba (ninaipaza)
Sauti ya Mungu wangu uliyonipa naipaza
Sauti yangu ninaipaza