MGANGA (LIVE) Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2023
Lyrics
Mganga mganga
Mganga wa waganga ni Yesu
Mganga mganga
Mganga wa waganga ni Yesu
Nasema nimemwona Mganga wa waganga
Anayeinamiwa na waganga wote hata na wachawi pia
Wanaleta madawa yao hata na hirizi
Na wanatangaza maovu yote walotendea wanadamu
Huyu Mganga kazaliwa Bethlehemu
Kalelewa Nazarethi la ajabu ni mwana wa bikira
Mganga mganga
Mganga wa waganga ni Yesu
Mganga mganga
Mganga wa waganga ni Yesu
Jina la huyu Mganga kwa kweli lanishangaza
Kwa maana linalo nguvu nyingi kama Mganga mwenyewe
Lilipotajwa na Petero Tabitha akafufuka
Kiwete njiani akatembea kwa ajili ya hilo jina
Paulo na Sila wakasifu kwa hilo jina
Milango ya gereza ikafunguka kwa jina la mganga Yesu
Mganga mganga
Mganga wa waganga ni Yesu
Mganga mganga
Mganga wa waganga ni Yesu
Nguo za huyu mganga hata nazo zina nguvu
Mama aliyevuja damu alipenya katikati ya umati
Kaguza upinde wa nguo damu ikakatika
Yesu akamwambia imani yako ndiyo imekuponya
Baada ya kusulubiwa nguo za huyu Mganga
Hazingepasuliwa kwa bei yake zikapigiwa kura
Mganga mganga
Mganga wa waganga ni Yesu
Mganga mganga
Mganga wa waganga ni Yesu
Aaaah aah aaah
Mganga wa waganga ni Yesu
Aaah aah aaah
Mganga wa waganga ni Yesu