Naanza Upya Lyrics
- Genre:Bongo Flava
- Year of Release:2022
Lyrics
Naanza Upya - Smile The Genius
...
(Naanza upya)
Sio mbaya nikianza upya
Tabasamu langu lisikudanganye, hapa nlipo najililia moyoni, kikubwa ni uhai naiomba salama
Yah,
Haya mapenzi yasinichanganye, kwenye hili ushauri sitamani, moja haikai mbili ndo imehama
Nilipofikia, ni pesa peke yake itanisumbuaa
Acha niumwagilie moyo, niupe vitu vyake nibadili gia
Nashushia bia, nasahau yalopita najiliwazia
Ila pole Sana moyo najua Kuna mengi umeyapitia
Na nishawasamehe, waloniumiza, waloniliza, kwenye mapenzi naanza upya
Najitunza, nadunduliza, sio mbaya nikianza upya
Namshukuru Mungu, sasa nimetulizana, Staki stress
Nataka ku-enjoy, moyoni shwari Sina stress
Ni kazi tu na marafiki, nimetulizana, Staki stress
Nataka ku-enjoy, moyoni shwari Sina stress
Nimeamuaa niache kudanganya na kudanganywa, maana sku'izi mapenzi hayana mana, niache kula nipate kunenepeana eti niwaze mapenzi
Na, Staki nijizeeshe mi bado kijana, Kheri ntafute kibarua cha kufanya, Niwe shabiki wa mpira tu bora Sana tu, Nianze kubeti
Yule alonichiti, huko washamchiti, analizana na ulimwengu wa mapenzi
Hayasimuliki, yupo tiki tiki, amechokeana kidudu Cha mapenzi,
Nishasahau yalopita najiliwazia
Ila pole sana moyo, najua kuna mengi umeyapitia
Na nishawasamehe, waloniumiza, waloniliza, kwenye mapenzi naanza upya
Najitunza, nadunduliza, sio mbaya nikianza upya
Namshukuru Mungu, sasa nimetulizana, Staki Stress
Nataka ku-enjoy, moyoni shwari Sina stress
Ni kazi tu na marafiki, nimetulizana, Staki Stress
Nataka ku-enjoy, moyoni shwari Sina stress
Staki Stress
Sina stress