Segedance ft Rich Mavoko Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2020
Lyrics
Segedance ft Rich Mavoko - Darassa
...
Mzee wa Segedance
Kukaba kuiba kashazoea segedance
Ana ngoma zote samba vanga sidimba
Ukiingia anga zake umeyatimba
(Classic Music)
(Abbah)
Hadithi hadithi utam kolea
Huwezi kusimulia mvua haijakunyeshea
Take care huu siyo moto wa kuotea mimea
Jumba bovu litakubomokea
Usimchokoze mwache komando kalala
Akiamka biashara shaghala baghala
Mtu hasara wamezinga mabomu Mbagala
Akitinga home akitoka anaacha msala
Kaamkia stand hata bila safari
Kashazima zake data hana habari
Kutwa za watu machata kujikubali
Master I'm very plasta mtu huwa hajali
Nitakuingiza chaka usimweke dhamana
Alikolala leo siyo alikoamka jana
Hana usiku hana mchana hana maana
Mtu lawama hana team hana chama
Unakuja kutaste taste weka weka anachomeka
Kama unabet bet anachana mkeka
Wameshikwa na baridi wanatetemeka
Wamepatwa na mawenge wanaweweseka
Huyu bwana hana mzaha anapiga honi
Tena kabeba silaha kali kibindoni
Sema suit wana vumbi usoni
Tia mguu uende na maji mtoni
Anazijua njama, drama, utampenda
Anakuwa mnyama ukiinama
Ukiinuka amekwenda nawe eeh
Mzee wa Segedance
Kukaba kuiba kashazoea segedance
Wanamuita segedance
Dhuluma kupiga nyumbani, segedance
Siku nyingine kumekucha kwenye misele
Ye anawaza mbele maisha yatakuwa mtele
Stori zake chenga chenga nyingi kama Pelle
Kwa vitambo hajambo majigambo tele
Tunaishi nae kwa kimachalele mtaani
Kukaa sero kwake yeye ni kama maskani
Umri wake na matendo hayaendani
Jua kali cheki mwendo shati begani
Akiingia party kaharibu kaishia
Sio mtu kweli bandia bandia
Mambo yake ni kudandia dandia
Mkate anashushia na bia
Kichwa imewaka ti na anapepesuka
Hana muda wa kuoga anapaka mafuta
Muwekee vigingi chimba chimba na matuta
Hutomkuta maajabu ya Musa
Unakuja kutaste taste weka weka anachomeka
Kama unabet bet anachana mkeka
Wameshikwa na baridi wanatetemeka
Wamepatwa na mawenge wanaweweseka
Huyu bwana hana mzaha anapiga honi
Tena kabeba silaha kali kibindoni
Sema suit wana vumbi usoni
Tia mguu uende na maji mtoni
Anazijua njama, drama, utampenda
Anakuwa mnyama ukiinama
Ukiinuka amekwenda nawe eeh
Mzee wa Segedance
Kukaba kuiba kashazoea segedance
Wanamuita segedance
Dhuluma kupiga nyumbani, segedance