Dunia Tunapita Lyrics
- Genre:Bongo Flava
- Year of Release:2022
Lyrics
Chorus
Kama mola kables saidia,
Uwezi jua kesho yako ulichoandikiwa,
Kama mola kables saidia,
Uwezi jua kesho yako utapoangukia,
Tuache kiburi cha uzima duniani tunapita tu,
Tuache kiburi cha uzima duniani tunapita tu.
Verse1
Aaaah mola eeh mola baba mola eeh,
Aaah mola eeh mola baba mola eeh,
Kumeshakucha nkasake shilingi mie,
Mana nimeamka sina ata sumni mie,
Mola apagui ridhiki ya we na mie,
Kama nimefungwa vifungo nifungulie,
Kabla hujatoka mja unatuia nia,
Mambo magumu ndo nehema inakaribia,
Kama yule wa kwanza na wewe utafuatia aah mungu atakusimamia,
Mola akikupa si ujanja wako usidharau wengine kwa kipata chako,
Me nawajua machawa wako mifuko ikitoboka imekula kwako.
Chorus
Kama mola kables saidia,
Uwezi jua kesho yako ulichoandikiwa,
Kama mola kables saidia,
Uwezi jua kesho yako utapoangukia,
Tuache kiburi cha uzima duniani tunapita tu,
Wewe na mimi tunapita tu,
Tuache kiburi cha uzima duniani tunapita tu.
Verse 2
Aaah mola eeh mola baba mola eeh,
Aaah mola eeh mola baba mola baba mola eeh,
Tuishi kwa hofu ya mungu tusipitilize kujiamini,
Tukizitazama pua ndo utajua sisi wachini,
Tuishi kwa hofu ya mola tusipitilize kujiamini tukilitazama jua hatuna budi kumuamini,
Kuna kipindi utakosa na utalala njaa mola anajua,
Kuna kipindi utapata bata utakula mola anajua,
Aaah mola eeh mola mola baba mola eeh,
Aah nalia na mola mola baba mola ooh,
Mola akikupa si ujanja wako,
usidharau wengine kwa kipato chako,
Me nawajua wapambe wako mifuko ikitoboka imekula kwako
Chorus
Kama mola kables saidia,
Uwezi jua kesho yako ulichoandikiwa,
Kama mola kables saidia,
Uwezi jua kesho yako utapoangukia,
Tuache kiburi cha uzima duniani tunapita,
Tuache kiburi cha uzima duniani tunapita tu.
Outro.........
Hakuna cha bekaflavour duniani ninapita tu,
Hakuna cha gari ata nyumba itabakia,
Hakuna cha moodewji duniani anapita tu,
Hakuna cha pesa umaarufu utabakia,
Hakuna cha bakhresa duniani anapita tu,eeh eeh
Hakuna cha gsm duniani wanapita tu,
Hakuna cha simba duniani anapita tu,
Hakuna cha king kiba duniani anapita tu yoooh,
Hakuna juma lokole duniani anapita tu,
Wala carry mastory duniani anapita tu udaku wote utapotea,
Mwijaku mzee wa kuchonga nae anapita tu yeeh yeeh,
Doctor kumbuka nae anapita tu,
Soud brown mzee wa mbanga nae anapita tu,
Kwisa mzee mkavu nae anapita tu.