9 pm Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2023
Lyrics
Saa inasoma 9 pm..
Nimechill maskani...
Simu inaita cheki namba ni unknown...
Shaisave majina kibao, mapenzi aliyeleta nani?
Nilifuta tu kinafiki, ila bado ipo kichwani..
Ubaya ni yule aliyekusahau,we daily unamkumbuka..
wakufanya uenjoy kafanya kumjua unajuta...
Kujifunika shuka wakati kunakucha....
Ubaya nikisema nimchukie nafsi bado inanisuta..
Napokea nasikia analia..
Huku sauti ya kiume pembeni inamkaripia..
Nahisi ni yule mchizi me, nayemchukia..
Aliye fanya huyu binti akanikimbia..
Binti niliyempa kila kitu..ye ndo alifungua hii zipu.....
Nilijua ataheshimu Nilimkuta hana kitu...
Kumbe mtaani wanapiga ubaya yeye ndo anawabipu...
Anabebwa kirahisi ni mwepesi kama tishu....
Hey mamy, so whats the plan now...
Akasema Jesse am sorry but sjui nianze how..
Nkamwambia comeback home, let settle this..
Chukua usafiri njoo home fanya upesi...
Nilimpa mapenzi,
Nilimpa cash..
Sikumfanyia ushenzi,
Sikutaka kuona anastress...
Nilifeel ye ni bless...
Kafanya niyachukie mapenzi..
Kanichuna sana cash..
Kanifanyia ushenzi..
Ameniacha na mastress..
Alikuwa mkosi sio bless..
Kaja kuharibu tu chorus ila kanyoosha versi..
Hakuna alichokosa... Kila kitu alipata..
Nishafunika sana makosa.. Mwingine angeshamuacha...
Sikutaka kumkosa..mtoto akichafua mkono siukati nauosha....
Kosa la msamaha inafanya kukosea tushindwe ogopa...
Alirudia nilirudia kumsamehe sikuchoka...
Niliumia nilivumilia maumivu ya kuyatosa...
Kaniacha nalia, mtoto wa nyoka ni nyoka..
Mara ring ring kwa phone..
Kwa geti nasikia honi..
Natoka nafurahi nachokiona machoni....
I see beautiful lady aliyenikalia kooni...
Naumia nachofeel moyoni..
Men why she was gone...
Kwani huu upendo hauoni..
Mabaya yake hayamchomi...
Akanipa hug machozi mashavuni..
Kilio cha kwikwi juu ya kifua cha mhuni...
And she say.. she miss me
Nawish ningejua what next...
Nisingepata hii stress...
Nawish ningejua what next..
Nisingeipata hii...
Nilimwambia feel at home karibu ndani...
naclear dereva uber nakufatia msosi mgahawani...
En stop crying stay cool wasigundue majirani...
Sikujua nakaribisha nuksi ndani...
Why Nilikubali kupokea mkosi..
Mi Nilivotoka kufata msosi..
Mungu kakosea kuificha kesho....
Sikumfanya chochote nimerudi mtoto kafia ghetto...
Alikuja kujiua kwangu,niibebe kesi.. (I don't know)
Au kala kipigo kwa yule boya pale ndo amekata gesi.. (I don't know)
Au ni mipango ya Mungu ambaye hakosei I guess... (I don't know)
Saa inasoma 3 AM, Questions on mahead....
pingu on ma hands....
Ndani ya cha Kituo police..
Na sijui what Next...