Minya Lyrics
- Genre:Trap
- Year of Release:2023
Lyrics
Usifanye kwasababu yao mandezi,
Mguu wako we hauwahusu ndezi,
Fanya kwaajiri yako we
Fanya kwaajiri yako we
Fanya kwaajiri yako we
Usiruhusu maisha yako yaendeshwe,
Minya
Yule mwana asiyekufaa,
Minya
Yule mwana anayekuloga,
Minya
Usimwoneshe zako pendwa njia
Usimwambie yako kubwa nia
Muoneshe yale unapitia
Muumize kichwa unavyoipata keki,
Apate homa anapoifunua neti,
Achane mkeka kila droo eti,
Akose vumba akose jibu beki,
Afie benchi kwa ulofa wa kichwa,
Alioujaza umpasue kisha,
Umzike hai mchafua misa,
Mchafua picha hafai kuikuza rika,
Ukifanya yale unayoweza unayopenda utajijenga,
Ukifuata yale wanayosema walimwengu utapotezwa,
Tena
Hautokuwa wewe hautokuwa mshindi hautokuwa bingwa,
Yaani wewe
Utashindwa kila kitu kwasababu sio wewe umefuata usiyoyaweza mpendwa,
Yote haya zingatia we,
Minya choyo, minya nafki ,minya ongo, minya chawi, minya zushi, minya fala ndani yako usifuge upuuzi,
Minya choyo, minya nafki, minya ongo, minya chawi, minya zushi, minya fala ndani yako usifuge upuuzi,
Minya aah aah
Minya aah aah
Wataua ulichonacho ukiwapa nafasi watawale akili yako,
Wataua ndoto wataua imani imani iliyokupa macho,
Watataka wajue unakula nini unafanya nini wakati gani,
Unaenda wapi demu gani unammiliki kwa kitu gani,
Ndani yako una nini kwani, wasipojua tatizo wakijua tatizo pia ,
Hawa wapuuzi hawana koo jomba hawaoni soo mjomba kukumbatia upuuzi,
Kwao upuuzi ndo kubwa mboga, kwa upuuzi ndo uwapao pumzi,
Uwapao furaha ndani ya hili jumba,
Uwapao nafuu ndani ya zao pumba,
Uwapao faraja pale walipodunda,
Uwapao imani kutoboa mpaka ndumba ,
Uwanyimao baraka ndani ya zile kuta,
Wawekee mipaka wasikuzoee kipuuzi wasiijue namba ikupayo pumzi,
Wasikujue ndani nje ndani wape upofu waikose chumvi,
Wape vyepesi warudi nyuma wakose kiini kikupacho pumzi,
Wakose misingi uliyoiweka juzi wakose raha uivutapo pumzi,
Wakose amani hata wakimnunua refa wakose ushindi mbele yako ninja,
Waloge walogavyo watabuma tu ushindi lazima mbele yako bingwa,
Yote haya zingatia wee
Minya choyo,minya nafki, minya ongo, minya chawi, minya zushi, minya fala ndani yako usifuge upuuzi,
Minya choyo, minya nafki, minya ongo, minya chawi, minya zushi,minya fala ndani yako usifuge upuuzi,
Minya aah aah
Minya aah aah
Walimwengu hupenda kuona ye mvuvi na we mvuvi ye paka na we paka ila sio we mtunzi ye mpuuzi .