Fikra Tulivu Lyrics
- Genre:Trap
- Year of Release:2023
Lyrics
Nafanya vile wasivyofanya vile vile,
Nafanya vile wasivyozoea vile vile,
Nafanya tofauti mmh!! tofauti,
Nafanya nje ya box mie vile,
Niko mbali nigger niko na safari,
Usinifuate mpuuzi huku niliko ni hatari,
Huku niliko ujinga haukumbatiwi,
Huku niliko uoga haupigwi kiwi,
Huku niliko fikra zetu ziko huru na nuru ya kuuvusha umati,
Kuulisha umma juu ya mawe kuupa shati koo la Big au Pack,
Ubunifu kwetu nguzo kuu huku niliko,
Ubunifu kwetu taa ya kichwa tusifike Kule siko,
Ubunifu njaa ya kila mpambanaji mfuata wito,
Ka Pac ao Newton wa flow napika diko,
Najaza mito haipotei haingojei msimu wa mvua haingojei,
Haipotei kiangazi haipotei singojei misaada singojei,
Siishi kwa nguvu ya jirani vitani ntashindwa kuishinda vita,
Ntashindwa kufurahi bila kilevi ntashindwa kutabasamu bila kupigwa picha,
Bila fikra tulivu mvivu angevimba kichwa,
Angeshindwa kuunda ndege alafu asingeng’amua undani wa FIFA,
X kutoitwa tiki Nike kutoitwa Fubu,
Fubu kutoitwa Reebok, peacock isingelaza mzungu,
Siongopi fikra mfu isingelileta dubu,
Isingeileta Nala , Facebook wala isingekuwepo YouTube,
Ubungo kusingekuwa na interchange mengi yangekufa ndugu,
Yangekufa kwa nimonia mamia ya wagonjwa wangekufa Bunju,
Ni rahisi kutumia nguvu kuliko akili hii iko wazi ndani ya hii nyumba,
Huwezi kwenda mbele bila changamoto,
Ili ufike kilele lazima changamoto,
Vunjabei asingevunja bei asingekuwa vunjabei hapa mjini asingeshika bunda,
Fursa ziko nyingi ziko ndani ya uwezo wako uwezo wako umeuzima Buda,
Hauwezi kuwa wewe kuwa wewe bila kujijua bila kujitambua kupoteza muda,
Huwezi baki chini ka ukijituma ka ukijituma huwezi baki chini dadeki dadeki,
Huwezi panda juu ka hujitumi ka hujitumi huwezi kuwa juu dadeki,
Sina masihara na hili jambo nifanyalo hivi nifanyavyo ndivyo inavyotakiwa dadeki,
Mabeki mnikabe mabeki mjipange kazi ngumu kunikaba kazi ngumu kwenu mabeki,
Sina hofu nanyi mabeki,
Koo langu funguo chuo kikuu dadeki,
Sifosi mtaa uitwe mimi,
Nafosi njaa ikose sehemu ya kukaa hapa mjini,
Sichoki kuulisha ubongo wangu upate afya,
Sichoki kufanya utunzi tungo zangu ziko tafu sana,
Tamu sana, fikra Pana, uaminifu dili kubwa sana,
Acha uzuzu kuwa mpana, kuwa mpya kila siku kukua sana,
Ki hip hop hii hip hop,
Ki hip hop hii hip hop,
Ki hip hop hii hip hop,
Ki hip hop hii hip hop,
Huwezi kwenda mbele bila changamoto,
Ili ufike kilele lazima changamoto,
Fursa ziko nyingi ziko ndani ya uwezo wako uwezo wako umeuzima buda.