Bora Peke Yangu ft. Rayvanny Lyrics
- Genre:Bongo Flava
- Year of Release:2021
Lyrics
Bora Peke Yangu ft. Rayvanny - Macvoice
...
(Next Level Music)
(Eiyoo Trone)
Heshima na upole wako
Ndiyvo vikanivuta kwako oh oh
Tabia na mwenendo wako oh
Vikanifanya nikupende eh eh
Kumbe mapenzi ni nyakati yanachanganya
Yakipoteza ramani wewe
Kitabu cha upendo wa dhati umechanachana
Haupo kama zamani wewe
Ngoma ikivuma mwisho wake hupasuka
Yote ya nini tuje kushikiana chupa
Wewe ukipanda kila muda mi nashuka
Oh ooh oh, oh oh oh
Message za watu wako na simu zako
Naona ila namezea tu
Najua machafu yako mabaya yako
Yanachoma mi napotezea tu
Kugombana mi siwezi
Nikwambie yote sababu ya mapenzi
Tena narudisha jezi nitulie
Ligi ya mapenzi siwezi
Kwako wewe, bora peke yangu
Nibaki peke yangu
Bora peke yangu
Niishi maisha yangu
Bora peke yangu
Nibaki peke yangu
Bora peke yangu
Niishi maisha yangu
Uliweka pamba masikioni
Husikii huoni ninavyoumia moyoni
Purukushani asubuhi jioni
Matusi mdomoni hata aibu huoni
Ukadanganya unaenda sokoni
Kumbe yuko mgongoni kitandani ukingoni
Una wapenzi wengine kinondoni
Hadi Kigamboni na Kariakoo shimoni
Ah wee, kumbe ni mnyama ulioficha makucha
Hata sura yako inakusuta
Nyama ndani ngano nje kama sambusa
Barafu wa moyo umeyeyuka
(Oh wo wo wo wo, oh wo wo wo wo)
Hukunipenda, pengine nilikulazimisha
Sawa nakwenda, japo sina wa kuninyamazisha
Huna makosa najilaumu nini?
Nilikupenda kwa nini?
Ona tu kugombana mi siwezi
Nikwambie eti sababu ya mapenzi
Tena narudisha jezi nitulie
Ligi ya mapenzi siwezi
Kwako wewe, bora peke yangu (bora peke yangu)
Nibaki peke yangu (ooh oh)
Bora peke yangu (ooh bora)
Niishi maisha yangu (niishi maisha yangu)
Bora peke yangu (bora peke yangu)
Nibaki peke yangu (nibaki mwenyewe)
Bora peke yangu
Niishi maisha yangu
Ah Niishi maisha yangu
Bora peke yangu
(Nusder)
(Added by Fidelisbzm01)