Tukipendana ft. Rado Kiraka Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2021
Lyrics
Tukipendana ft. Rado Kiraka - Momumo
...
Blaack. Maagician
Oii uuh
Naona Chuki,Ubinafsi Na Dhiki Zimejazana/
Sijaona kikwazo Kipi, Kama tu Tukipendana/
Kutofautiana,Haina maana Kugombana/
Kama tukishirikiana Tutafika Mbali Sana/
Upendo ndio Maisha,Faraja Kwenye Lawama/
Malengo Yakitisha,Ina maana utakazana/
Tuepuke Kabisa,Vinyongo Na Uhasama/
Sambaza Maarifa kwa Vitendo We Kijana/
Usizitake Sifa Kwa Skendo Na Kubishana/
Vipi Ka Tukipendana?Vipi Ka Tukisaidiana?
Madaraja Tutajenga Yatuvushe Tunapokwama/
Tuongeze Miaka Kenda, Maana Chuki Inatafuna/
Itikadi Tofauti na Sote Watanzania/
Vitisho Na Bunduki,Sio Misingi Iliyotulea/
Bado Twahitaji Kujua,Wapi Ndugu Walopotea/
Pamoja Tutatambua, Huku Wapi Twaelekea/
Vipi Ka Tukipendana??
Yeeah
Vipi Ka Tukipendana?
Ya ya ya
....(What If We Love Each Other?)
Vipi Ka Tukipendana?
Let's All Love Each Other)
Vipi Ka Tukipendana?
uuh...
Kama ziumiazo Ni Nyasi,Tembo wanapopigana/
Watoto waende Wapi,Mkiachana Baba Na Mama/
Nani atabaki Mwema,Mkitupiana Lawama/
Wana Watarithi Chuki,Matusi Na Kugombana/
Vipi Ka mkipendana,heshima Na Kusameana/
Amani Itatawala,Umoja Kushirikiana/
Tukumbukane kwa Sala Utu na Fikra Njema/
Tusisubiri Misiba,Tupendane (I) ngali wazima/
Za nini Mali bila Upendo Na Furaha/
Hutozikwa Na Gari Ama Cheni Unazovaa/
Chuki unazohubiri,Hazitojenga Mitaa/
Mwenzako akifeli,Sio kwamba utapata Raha/
Penda Kutenda,Unavopenda kutendewa/
Tenda Unachopenda,Kwa Upendo Na Sio hila/
Badili mwenendo,Ni mapema Hujachelewa/
Mapendo sio Magendo,Hayana Hasira wala kuzira
Vipi Ka Tukipendana??
Yeeah
Vipi Ka Tukipendana?
Ya ya ya
....(What If We Love Each Other?)
Vipi Ka Tukipendana?
Let's All Love Each Other)
Vipi Ka Tukipendana?
Yeaah Makantani Acha Upendo Utuongoze..
Yeaah..
Naikanyaga Laki,Nasimama ndani ya Haki/
Nawaona Mawaki,Wanapangwa Kama mishkaki/
Nataka Tuheshimiane tuzo ya pombe Siitaki/
Kwa Mkuu Tumuombe Atubariki/
Za Hatimiliki,Hazitimiliki Cha Mtu kamwe Hakiliki/
Hawana Usalama,Ndo maana Siri zao zina-leak
Stori zao za nyuma,wanazificha hawazianiaki
Nimeshakuwa mtu mzima,Ngumu yangu Hailainiki/
Already got One idont need no More mic...
Vipi Kama Tungependana Wanangu wa Handakii..
Magiciaan Momumo Makantani Viraaka
Oii Oiii
R.I.P MKOLOSAE