Sijashindwa Lyrics
- Genre:Bongo Flava
- Year of Release:2019
Lyrics
Sijashindwa - Momumo
...
Yeah
Uuh Aa
V1.
Sijashindwa Kuandika, Kwa Uhakika Na Fasihi,
Wengi Marapa Wa Marapa, Wameisahau Jamii,
Sijashindwa Haya Maisha Usidanganywe Na Tv,
Siogopi Dhihaka, Rohoni Nina Utii,
Sina Mashaka, Ninapofeli Sijutii,
Najifunza Kipya Daily Naongeza Bidii,
Nawaskia Nawaambia Wanajifanya Hawaskii,
Inapokuja Kutokea "ANAJIFANYA NABII "
Sijashindwa Watoto, Kila Kona Ya Mtaa,
Kuna Vya Moto, Usiziendekeze Zinaa,
Zinazimwa Ndoto, Kwa Sababu Ya Njaa,
Na Tamaa za Masaa, za Kudaka Hizi Chapaa,
Sijashindwa Msoto, Nikamate Silaha,
Stress Zikizidi, Zinipeleke Bar,
Nidiss Wengine Wanione Mi Shujaa,
Nipate Sifa Bila Bars...
Bila Bars.. Bars
Hook... .
Sijashindwa Kuandika, Kwa Uhakika Na Fasihi,
Uuuh
Wengi Marapa Wa Marapa, Wameisahau Jamii,
Wameisahau Jamii...
V2.
Sijashindwa Kuwa Nawe, Mamacita Binti Afrika,
Umezidi Ukwale, Kila Kitu Unataka Shika,
Kila Sehem Unataka Pita, Mwisho Uzue Patashika,
Kuchanganya Mabwana, Unachojali Pesa Sifa,
Sio Kwamba Uzuri Huna, Ila Umekosa Maarifa,
Umejazwa Taarifa, Zisizothibitika,
Badili Mwenendo, Ukitaka Badilika,
Mapendo Sio Magendo, Hayahitaji Kujificha,
Yooh
Sijashindwa Tukana, Nionekane Mi Natisha,
Nionekane Mi Ndo Kichwa, Na Uwezo Wa Kuandika,
Sipo Kubadilisha, Nimetumwa Wakilisha,
Kitaa Kimesizi, Na Machizi Wanatabika,
Kipato Hakikidhi, Hili Ni Deni La Taifa,
Usipigane Na Wenzako, Pigana Na Maisha,
Pambana Umiza Bichwa, Inuka Chakarika,
Hakuna Wa Kukuvusha, Usipotaka Kuvuka,
(KnowThyself)
Hook...
Sijashindwa Kuandika, Kwa Uhakika Na Fasihi,
Uuuh
Wengi Marapa Wa Marapa, Wameisahau Jamii,
Wameisahau Jamii...