Nijaze Lyrics
- Genre:Afrobeats
- Year of Release:2020
Lyrics
Nijaze - Janet Otieno
...
Uuuh..
Roho Mtakatifu.. Wewe pumzi ya moyo
Roho Mtakatifu njoo utawale
Wewe uliyeju ya yote
Ninakuomba utawale
Nataka nizame ndani na ndani zaidi..
Zaidi ya fahamu zangu
Na sura yako iumbike kwangu
Mapenzi yako yatimizwe
Uwepo wako uwe fungu langu
Ninapendezwa sana nawe
Ewe roho wa Mungu
Fanya makao ndani yangu
Wewe pumzi yangu
Fanya makao ndani yangu
(Nijaze [×3] - - Bila kukoma){×2}
Mwalimu wa walimu
Nifunze leo
Nisiwe kikwazo cha uwepo wako
Sitaki hisia zangu ewe Roho
Zisiwe kikwazo ya nguvu zako
Rejesha kiu yako nikutamani zaidi
Fungua sikio langu nikusikie zaidi
Maana... Hakuna kilicho na thamani zaidi yako
Hakuna... Aliye na hekima kama yako
wewe huchunguzae mawazo ya mtu
Naomba u Nijaze leo
{Ewe roho wa Mungu
Fanya makao ndani yangu
Wewe pumzi yangu
Fanya makao ndani yangu
(Nijaze [×3]--Bila kukoma){×2} } X2