Nakuabudu Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2014
Lyrics
Nakuabudu - Faustin Munishi
...
e mungu wangu nakutukuza wewe
nakuabudu pokea sifa (ni wewe pekee..)
ni wewe pekee binguni na duniani umeenea unatawala (nikipumua)
nikipumua(baba) uweza na nguvu zako
zinabubujika moyoni mwangu (niseme nini) niseme nini e... ila ninakushukuru fadhili zako ni nyingi muno
(uwepo wako) uwepo wako nausikia karibu magonjwa yangu yanayeyuka
(wewe ni moto) wewe ni moto (baba) wakuunguza shetani akikuona anatoraka
(najisikia) najisikia mwepesi mwilini mwangu uzito wote umotoweka
(na roho yangu) na roho yangu nakuinulia wewe furaha yangu machizi yangu (e.. baba yangu) e baba yangu (ah..) nashindwa kuvumilia yanadondoa machoni mwangu
(sina huzuni) sina huzuni ni machozi ya furaha (eh) ni machozi ya furaha umeniponya nina uzima (nilizunguka)nilizunguka dunia kila mahali sikumpata wakuniponya
(nilipoteza) nilipoteza hazina na pesa zangu na msaada sikuupata (na sasa hivi) na sasa hivi nimekutukuza wewe umeniponya bila bila malipo (wewe ni mungu) wewe ni mungu (baba) ufananishwe na nani akuna kote ni wewe pekee (ni kimbilio) ni kimbilio wakati wa matatizo ngome imara ni msaada (ni jemedari) ni jemedari adui watesi wangu umepambana wametoweka (wakiniona)
wakiniona wasema kama si wewe wangenimeza ? (upendo wako) upendo wako umenizunguka kote kama bahari sionekani (si mimi tena) si mimi tena ninayeishi mwilini bali ni wewe u ndani yangu (uhai wangu) uhai wangu nilionao mwilini si mali yangu (baba) ni mali yako (na mwili wangu) na mwili wangu ni hekalu lako wewe na hauko mbali uko na mimi ( huduma yangu) huduma yangu ni wewe uliyenipa niitumie babakuinua (ninapoita) ninapoita wanisikia unibariki nakuomba (uniongezee) uniongezee hekima na maarifa nitunge nyimbo za kukusifu (ni wewe pekee) ni wewe pekee
binguni na duniani umeenea umetawala
eeeh mungu wangu ninakutukuza ninakuabudu pokea sifa wewe pekee
mbinguni na duniani
umeenea unatawala
nikipumua uweza na nguvu zako nabubujika moyoni mwangu
niseme nini ila nakushukuru fadhili zako....