Mungu Mtakatifu Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2013
Lyrics
Mungu Mtakatifu - Reuben Kigame
...
Eh Mungu wangu
Jehova Baba
Uliniumba nikuabudu
Uhai wangu
Maisha yangu
Nakukabidhi Eh Mungu
Jina lako Lina nguvu
Mkono wako watenda makuu
Mimi nitasifu haki yako
Na wema wako
Eh Baba
Wewe ni mungu mtakatifu
Mbingu na nchi zimejawa
Na utukufu wako
Wewe ni Mungu Mtakatifu
Kwa uwezo wako Ukaniumba
′Kanipa uwezo kutawala (usifiwe baba)
Viumbe vyote
Ulivyoumba
Utukuzwe Eh Mungu
Mimi Baba
Ni kitu gani
Unanijali jinsi hii
Ulimtuma mwana wako
Akanifia
Eh Baba
Wewe ni mungu mtakatifu
Mbingu na nchi zimejawa
Na utukufu wako
Wewe ni Mungu Mtakatifu
Milele yote nitakusifu (Mungu Mtakatifu)
Kwa fadhili zako Mungu(oh oh oh)
Sitoacha kulitukuza(Jina lako Baba)
Jina lako Ewe Mungu Mungu wangu oh oh oh
Wewe ni mungu mtakatifu
Mbingu na nchi zimejawa
Na utukufu wako
Wewe ni Mungu Mtakatifu