Halali Jalali Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2023
Lyrics
Eh Bwana hata lini utanisahau mimi nashangaa hata milele
Hata lini utanifichia uso wako Bwana wangu ninauliza
Hata lini nifanye mashauri mimi moyoni mwangu maskini mie
Nikihuzunika na kufadhaika mwenzenyu mchana kutwa a
Je hutaniitikia hata nilalapo usingizi wa mauti i
Yamenifika sehemu hofu yanitawala nawe hutoitika
Hata hivyo nitatumaini maana ni hai wanirai mimi niamini
Kwani harandirandi mja wa Jalali miongoni mwa walala hoi upo
Japo najihisi pekee ni ahadi yako mwaminifu utamtunza
Nami nifunze kuulinda subira
Halali jalali kila ninapo pitia mikononi mwao watesi wangu
Na hali ya maisha ijapo kuwa ngumu sana sibanduki miguuni pake mimi
Sifa sifa nitatuma kwake na kumtumaini ninajua nia yake kwangu daima nzuri na hatonitenga mimi
Hivi tavumilia yeye yu nami aliye pendo siku zote