Mistarillionaire Lyrics
- Genre:Afrobeats
- Year of Release:2018
Lyrics
Mistarillionaire - King Kaka (Rabbit)
...
Kwa game wangapi nime waingiza kama coni au gyna
ata nikiwapea my rhyme book hawawezi panda ka designer
hii kuku sita ichinja ina bahati ime taga
na mi sio warrior na hesitate yule ali hesitate alisha aga
oh yee of little faith na dhambi mingi siku hizi ndani ya dini
mi ndio marking scheme aisee na boil down kwa my ulimi
hiyo ship ilisha sail ati chai sikuizi iko kwa sachet
na maziwa imekuwa unga, unga imekuaje uji
hii world iko confusing,
after homo erectus I think evolution imeenda kwa mbuzi
ma dark-skin wana bleach na wake wana ficha uchi na uzi
pastor ana kunywa makali na maji ndio aweze ku preach
wengi watasema nawaonea wengine watasema nawa chomea
na wale wako kwa hii stori watajitokea
juu wanajua si mistari tu ni mistarillionaire
Kuna tu yaliyopita hakuna sasa lakini kuna ya kesho
niliambia mama sikuizi mi danger
painter anachora picha na maneno
opening leo gallery yangu iko kwa ma tenje na mathree
mtaani hadi kwa ma tecno na matendo
kuna time nilicheki bank and I had five million like it's nothing
nika tbt siku we had nothing, nothing to live for
so tulikuwa tuna live for?
tulikuwa tu tuna live na we were four
me my mom and my bros
kwa room ndogo pale marish
tukiwa na ndoto ya room so
nilikuwa tu na jichocha time nili do ligi soo
I was growing nikiwa mdogo benjamin buttons
after two months nilikataa maziwa
nilijua kidogo macho yangu bado white
bado nilikua mpure
yaani sai mna pigania kiti ya king na compareiwa aha
kijiji yote ina niombea we endelea wivu
ndio mna nionea
na sio mistari tu ni mistarillionaire
Maali imefika nisha gundua hawa watu wana vision fupi kama asians
na ambition yangu kuna time wali confuse na impatience
nilikuwa na no pen no biro nika rudi drawing board
nukta nukta tone tone picha ikawa wazi after nime connect dots
binadamu wengi wako on a leash sio mbwa tu
unadhani omena sio fish shairi ina tungwa tu
notice na sundo tu vako ya ark ya Noah two by two
niliwacha kua inspired na wao niko inspired na family kwa hao
naulize Mrs Wakaba mi classic wa malenge
even though mum alikuwa anauza maembe na malenge
wacha vile sai mna niona kwa ndege
wananionea gere mi genge mi ndani ya tenje
wacha usenge pale akala sio usengee
vipofu wao wanipatie nta wasomea
sio mistari tu ni mistarillionaire
Kuna conference Nairobi naskia wana funga njia
wana discuss vile wata fund vita
sijui kama wameskia kuna wenye wamekufa njaa Mvita
Isiolo na Mandera maduanzi si waashe antenna
wajaze lori sai sai wacha vile wana advertise free wifi
same flower different colors
rose ya nyeupe na red ina maana tofauti
maisha kuzaliwa leo baadae ni mauti
uwe na pesa ngapi huwezi nunua jana
huwezi bribe Mungu akuonyeshe kesho
bado waswahili huni zingatia wameeka mistari zangu kwa leso
ma concorde na deal na wao sikuizi ni ma sailor na ma hostess
went from kusanya BMX to ndoto za kuendesha Porches
nguvu za Luanda Magere kwa kivuli mi God ndio coaches
na it's obvious hakuna journalist ako na swali moja
bado wana jifunza the art ya sahani moja
nawa rogea rogea time nili bobea bobea
na sio mistari tu ni mistarillionaire
Una ongea story ya mkate na dush story ya cheese na paka
una make moves na nyoka I guess it's too late
maisha ime mpeleka shule
8 4 4 4 4 ndio maana school fees bure
kulikuwa na Kennedy to Sunguch then Kaka Sungura to Rabbit
to King Kaka delinquent I say pasa liquid
nisha pata wengi wa kuni pea na wengi wakuni nyima
umbea ungekuwa mmea tungekua ma tycoons na wakulima
tv imejaa wahuni radio imejaa matapeli
niacheni pia mi ninone ka juwao paka ya hoteli
sichezi but nacheza my cards right
nyinyi joker mi ni stalker nyi mko in the nick of time
mi niko ma nickel and dime
niko studio na rhyme niko close to my prime
ambassador wa eastlando ndani case study ya walami
mi niko nyumbani mi ndio fani mi ndio mixtape ya E-sir na vitu flani
mi ndio hujaza sahani mi ndio king na si na samahani
mi ndio joto ya winter na njeve ya summer yaani
mistari barabara pokea shamrashamra
book yangu haina cover utani judge aje
nime waalika kifo ya career yenu mta dunga aje
since mnajifanya wajuaji wata juaje
mi ni kiziwi huskiza the silence
kipofu ana ona the future through my cornea
na sio mistari tu ni mistarillionaire