Loading...

Download
  • Genre:Gospel
  • Year of Release:2015

Lyrics

Mv Bukoba - Hedaru Central Church SDA Choir

...

Ilikuwa tarehe ishirini

na moja mwezi ule wa 5

mwaka elfu moja mia tisa tisini na sita ndugu zetu wapendwa

waliianza safari yao

katika usiku wa manane

walipokaribia kufika kulikuwa kumeanza kupambazuka alfajiri

na mataa ya mji wa mwanza-alfajiri

yalishaanza kuonekana - alfajiri

wasafiri wote wakawa na tumaini kuwa watafika salama,

wengine walilala usingizi

na wengine walikunywa pombe,

wengine walifikiria kuuza biashara zao wakifika mwanza.

wengine walilala usingizi

na wengine walikunywa pombe

wengine walifikiria kuuza biashara zao wakifika mwanza.

Ndipo tufani ikatokea,

meli ikapigwa na mawimbi

ikaanza kuyumba na kuyachota maji na mwisho ikaanza kuzama,

watu wakaangua vilio,

wakiuhitaji msaada,

zikafika boti za wavuvi kuwasaidia lakini hazikutosha kabisa,

waliookolewa wachache - Kabisaa

wengi wakafa ndani ya maji - Kabisaa

waliokufa ni masikini na matajiri wenye vitu vyenye thamani,

walijaribu kutoa fedha

ili wapate kuokolewa,

hawakupata mtu wa kuzipokea wakafa nazo kwenye mifuko.

walijaribu kutoa fedha

ili wapate kuokolewa,

hawakupata mtu wa kuzipokea wakafa nazo kwenye mifuko.

Na dunia hii

nayo ni sawa kabisa,

na meli inayosafiri baharini,

tumeshasafiri usiku wa manane

na alfajiri nayo imekaribia,

tumeshaiona bandari sio mbali,

lakini bahari nayo imeshachafuka,

na safari yetu imeshakuwa na mashaka

kwani chombo chetu kinapigwa na mawimbi sana.

Wewe ndugu!

ingia ndani ya boti ya yesu-ili

Ili uokolewe na ajali- Kwani

Kwani boti yake haina gharama yoyote.

Wewe ndugu!

Fanya uamuzi leo twende-ili

Ili tukaishi na mwokozi - ndugu

Katika nchi mpya mwokozi katungojea

Sasa njoo ndugu

tukatawale

Tukafurahie

mji wa raha

Tukaishi na yesu

Kule mbinguni

Nawe Baba

njoo leo tukatawale

Tukafurahie mji wa raha

Tukaishi na yesu

Kule mbinguni

Nawe Mama

njoo leo tukatawale

Tukafurahie mji wa raha

Tukaishi na yesu

Kule mbinguni

Nawe Kaka

njoo leo

tukatawale

Tukafurahie

mji wa raha

Tukaishi na yesu

Kule mbinguni

Nawe Dada

njoo leo tukatawale

Tukafurahie mji wa raha

Tukaishi na yesu

Kule mbinguni

Similar Songs

+

      -   or   -

      -   or   -

      NG +234

          Please Select A Playlist

          Add New Playlist

          Share on

          Embed: Love & Light EP

          Custom Size :

          • Default
          • Desktop(300*600)
          • Mobile(300*250)

          Type :

          • HTML/HTML5 (WordPress Supported)
          Get Boomplay Premium
          for
          Payment Method
          Pay With
            Review and pay
            Order Date
            Payment Method
            Due Today
            Flutterwave
              Subscription Successful

              Congratulations! You have successfully activated Boomplay 1 Month Premium.

              Now you have access to all the features of Boomplay App.
              Payment Failed

              Please check your balance and then try again.

              You'll lose your subscription if we don't have a working payment method for your account, so please check your payment details.
              Need help? Contact Boomplay Subscription Support.
              Payment Processing...
              10 s

              Payment is being processed by . Please wait while the order is being comfirmed.

              Payment Processing
              Your order is processing, and it may take up to a few days for the service provider to handle your payment. Please kindly stay tuned and check your order status in ‘User Center’.
              About Order Status