Ujio Wa Yesu Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2023
Lyrics
Alisema mwenyewe ya kwamba atarudi
Kuja kuchukua wateule
Waloshinda dhiki na taabu za dunia
Watakenda naye juu mbigunguni
Kila jicho litamwana bwana akirudi
Hata wale walio mchoma
Muda upo Fanya matengenezo Mpendwa
Yesu Yu karibu mlagoni
Anakuja Yu karibu
Kuchukua wateule
Kwendo nao juu mbinguni kutawale yuaja
Wito kwako Leo jiandae Acha dhambi
Tumlaki Bwana Yesu Mawinguni.
Mutukio yanayotokea hivi leo
Yaonyesha Bwana Yu karibu
Alisema tuonapo hayo yatukia
Tutambue Mwisho ukaribu
Heri wale wanaolisoma Neno lake
Na wale wanaolisikia
NaKutenda sawa sawa na Mapenzi yake
Kwao itakuwa ni furaha.