Sina Uende Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2022
Lyrics
Sina Uende - Komando Wa Yesu
...
Sina uende,sina uende
Rafiki yangu alinitembelea nyumbani
Miaka mingi mimi naye hatuonani
Amependeza si kama zamani
Nikampa hongera,hongera rafiki
Ndipo akaniambia siri ya mafanikio yake, mwili ulitetemeka sikuamini
Dunia ina siri,dunia hii jamani
Upewe macho uone
Ndipo akaniambia siri ya mafanikio yake, mwili ulitetemeka sikuamini
Dunia ina siri,dunia hii jamani
Upewe macho uone
Nikamwambia mimi nina Mungu tu
Baraka zangu zinatoka juu
Hata zichelewe nitasubiri tu,simama uende
Nikamwambia mimi ni Mungu tu namtegemea
Baraka zangu zinatoka juu
Hata zichelewe nitasubiri tu,simama uende
Hawaruki pamoja ndege wasiofanana
Giza na nuru haviwezi patana
Namwamini Mungu tena namwamini sana
Sina uende
Sina uende(Ni kweli 'mi ni kabwela)
Sina uende (Ila nitabaki na imani yangu)
Sina mimi la kufanya,sina uende
(Mungu ataniinua)Sina uende
(Mlicho nacho jua)Sina uende
(Sina,sina eeh) Sina mimi la kufanya,sina uende
Msaada wa mwanadamu una mwisho ujue
Msaada wa Mungu ni wa milele utambue
Bila huyu Mungu usijisumbue eti mambo yako yaende
Upendo wa mwanadamu huishia kaburini
Upendo wa Mungu ni wa milele utambue
Bila huyu Yesu usijisumbue eti mambo yako yaende
Anayeinua ni Mungu tu(Mungu tu,Mungu tu)
Anayebariki yuko juu(yuko juu,yuko juu)
Usisikilize ya watu,imara ishindwe
Hawaruki pamoja ndege wasiofanana
Giza na nuru haviwezi patana
Namwamini Mungu tena namwamini sana
Sina uende
Sina uende(kutumikia mabwana wawili)
Sina uende (Mungu wa kweli)
Sina mimi la kufanya,sina uende
(Ninachojua nitavuka ng'ambo)Sina uende,sina uende
(Najua Baba atafanya jambo) Sina mimi la kufanya,sina uende
(Iko siku yangu ya kung'ara)Sina uende
(Tena sina papara)Sina uende
(Bwana atanipa ishara)Sina mimi la kufanya,sina uende